MADA ZA AGRF 2023 ZILIZOJADILIWA SEPTEMBA 8



MADA ZA AGRF 2023 ZILIZOJADILIWA KATIKA KUMBI NDOGO ZA UKUMBI WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE, DAR ES SALAAM,

TAREHE 8 SEPTEMBA 2023

 

Imeandaliwa na Nyabaganga Daudi Taraba

Mada za hitimisho zilijadiliwa katika kumbi ndogo zilizopo kwenye maeneo ya ukumbi mkubwa wa Kimataifa ya Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Mada mbili zilijadiliwa katika siku hii ya mwisho wa kilele cha mkutano wa kujadili mifumo ya uzalishaji chakula barani Afrika.

Mada ya 1 ilihusu Ubunifu Katika Kuchochea Hatua za Kuchukuwa Kuhusiana na Mifumo ya Uzalishaji Chakula Himilivu kwa Mabadiliko ya Tabianchi.

Mada ilijadili uzoefu katika mifumo mbalimbali ya uzalishaji chakula inayotumika barani Afrika. Mjadala ulilenga kufanya maboresho katika mifumo hiyo ili kuweza kuwa na mifumo himilivu kwa mabadiliko ya tabianchi. Aidha, majadiliano yalifanyika kuhusu teknolojia zinazokidhi hali ya mazingira katika uzalishaji.

Waandaaji walikuwa ni CGIAR na FCDO

Wazungumzaji walikuwa ni kutoka CGIAR na Benki ya Dunia.

 

Mada ya 2 ilihusu Maendeleo ya Kilimo cha Bustani Nchini Tanzania

Katika miaka 10 iliyopita, kilimo cha bustani nchini Tanzania kimekua haraka na kuwa kivutio cha ajira kwa vijana na wanawake. Washirika wa Maendeleo nao wamebaini kuwa kilimo cha busatani kinatoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi.

Mada ilijikita kujadili uzoefu kutoka kwa Jackie Mkindi wa TAHA, Agriconnect (EU), Kilimo Tija (USAID) na DECIDE (NORAD). Kutokana na uzoefu uliopatikana, mjadala ulitoa mapendekezo ambayo yatajumuishwa kwenye taarifa ya jumla ya AGRF 2023.

Muandaaji alikuwa ni Agribusiness Market Ecosystem Alliance (AMEA).

Wazungumzaji walikuwa ni kutoka Agribusiness Market Ecosystem Alliance (AMEA), Tanzania Horticulture Association (TAHA), Agriconnect Program, Farm Africa (DECIDE Program), na Produce of Tanzania Co. Ltd (Kilimo Tja Program).


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post