Mkurugenzi wa Kampuni ya KEMANYANKI Nicholaus Mgaya akiongea na wakazi wa Nyamongo katika hitimisho la mashindao ya Kemanyanki CUP
Mbunge wa Jimbo la Tarime vijijini Mwita Waitara akiongea na wananchi wa Nyamongo katika hitimisho la KEMANYANKI CUP.
Selina Mkaro ambaye ni Afisa rasilimali watu kampuni ya KEMANYANKI akisoma risala mbele ya mgeni rasmi.
Wachezaji wakiendelea kusakata mpira ambapo Fainali imekutanisha Murit FC dhidi ya Kewanja Fc.
Na Cleo 24 Tv - Mara
Makampuni yanayofanya kazi na Kampuni ya Uchimbaji wa mawe yenye Dhahabu ya Barrick North Mara yameaswa kusaidia Vijana wanaozunguka Mgodi huo ili kuongeza uchumi kwa vijana hao.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa kampuni ya KEMANYANKI Nicholaus Mgaya kwenye kufunga tamasha la Michezo lililofanyika Nyamongo.
Kemanyanki amesema kuwa kampuni yake imetoa fursa za ajira kwa vijana takribani 250 ambao wanatoka vijiji 11 vinavyozunguka mgodi wa Uchimbaji wa Mawe yenye Dhahabu Barrick North Mara.
“Matarajio yetu ni kusaidia vijana kuondokana na changamoto za ajira sasa naomba makampuni yote tushirikiane”, alisema Nicholaus.
Afisa Rasilimali kampuni ya KEMANYANKI, Selina Mkaro amesema kuwa kampuni hiyo inafanya kazi na Mgodi shughuli za Usafi wa Mazingira,Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi, ufugaji wa Kuku wa Mayai, Ufugaji wa Nguruwe,na kuuza vifaa vya mitambo mbalimbali pamoja na shughuli za Ulinzi.
Aidha Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini Mwita Waitara ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kuwa Vijana watumie fursa za uwepo wa Mgodi wa Uchimbaji wa Mawe yenye dhahabu Barrick North Mara ili waweze kunufaika.
Kampuni ya Kemanyanki iliyopo Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara ni moja kati ya makampni yanayofanya kazi na Mgodi wa Uchimbaji wa Mawe yenye Dhahabu Barrick Noth Mara.
Hivi karibuni kampuni hiyo imeanzisha mashindano ya Mpira yanayojulikana kwa Jina la KEMANYANKI CUP mashindano yaliyoshirikisha timu 11 zinazotoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Uchimbaji wa Mawe yenye dhahabau Barrick Norh Mara Nyamongo pamoja na Timu moja ya Kemanyanki Fc, mpira huo ulikuwa unatimua vumbi kwenye viwanja vya Ingwe Sekondari.
Katika Mashindano hayo Kewanja Fc waliibuka kidedea kuwa mshindi wa kwanza dhidi ya Murito FC baada ya kutoka sare ya kutofumgana nakuamua kupiga mikwaju ya Penalti na ndipo Kewana waliibuka kidedea.
Mshindi wa kwanz Kewanja amepatiwa kiasi cha shilingi Laki saba na seti moja ya jezi, mshindi wa pili Murito FC amepatiwa shilingi Laki Nne na seti moja ya jezi, mshindi wa tatu ni Nyangoto FC alipatiwa shilingi Laki tatu na seti moja ya jezi na Mshindi wa Nne ni Nyabichune FC alipewa seti moja ya jezi.
Zawadi nyingine zilitolewa kwa Timu watoto chini ya miaka 15 ambao walishindana ambapo timu ya Nyamwaga ilikutana na Timu ya Kerende na Nyamwaha kushinda nakupewa zawadi ya shilingi elfu Hamsini na mpira mmoja huku Kerende Fc wakipatiwa mpira mmoja.
Awali kabla ya Fainali kulikuwa na michezo ya kukikmbiza kuku, kukimbia kwenye magunia, kuvuta kamba, kula nyama chomo, kula mkate na soda lengo ni kukutanisha vija na pamoja ili kuondokana na dhana za kuvamia mgodi huo mara kwa mara.
Social Plugin