Makao makuu ya halmashauri ya Chalinze
NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE
HALMASHAURI ya Chalinze Mkoa wa Pwani, imepokea jumla ya shilingi 2,222,000,000 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024.
Taarifa kwa umma iliyotolewa mapema wiki hii na kitengo Cha mawasiliano katika halmashauri hiyo, kiasi hicho cha fedha kimelengwa katika ujenzi wa Madarasa , Vyoo vya shule, vituo vya afya, zahanati na vifaa tiba.
Katika fedha hizo jumla ya shilingi 208,000,000 ni kwaajili ya Ujenzi wa Madarasa na vyoo katika shule kongwe za msingi.
Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa Madarasa na vyoo vya shule za Sekondari(464,000,000/=), ujenzi wa uzio wa shule ya msingi Chalinze shilingi 30,000,000 na ujenzi wa nyumba mbili za wakuu wa idara zenye thamani ya shilingi 320,000,000.
Halmashauri hiyo pia imepokea shilingi 100,000,000 kwa ajili ya umaliziaji zahanati, Shilingi 700,000,000 kwaajili ya uendelezaji wa hospitali ya Wilaya, Shilingi 300,000,000 kwaajili vifaa tiba katika vituo vya afya na shilingi 100,000,000 zimeelekezwa kwenye vifaa tiba vya zahanati katika halmashauri hiyo.
Social Plugin