Jojoo fun Park imeandaa Tamasha maalum ambalo litakutanisha watoto kutokasehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam kushiriki katika michezo pamoja na kujifunza mambo mbalimbali.
Tamasha hilo lililopewa jina la ‘Holiday Picnic’ linafanyika Jumamosi Septemba 9 kwenye ukumbi wa Jojoo fun Park, Kimara Bonyokwa ambapo mbali na michezo hiyo pia watoto watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ya afya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mratibu wa tamasha hilo, Dk Asha Mahita, alisema wazazi pia watapa fursa ya kujifunza namna ya kutambua kipaji cha mtoto.
Alisema kutakuwa na madaktari wa watoto ambao watatoa elimu juu ya umuhimu wa kuangalia afya ya watoto na ushiriki wao katika michezo.
“Tumeandaa Holiday Picnic ili kuwapa watoto a b c za afya na fursa ya wazazi kujifunza mambo muhimu katika malezi huku wakizingatia umuhimu wa afya zao,” alisema Dk Mahita.
Alisema moja ya mambo ambayo wazazi wanajisahau juu ya watoto wao ni kutowapa nafasi ya kushiriki michezo lakini pia kushindwa kufuatilia
taratibu za kuwapatia chanjo zinazohitajika kwa watoto kulingana na umri wao
“Chanjo ni mojawapo ya hatua bora zaidi za afya ya umma na kuokoa watoto.
Alisema moja ya mambo ambayo wazazi wanajisahau juu ya watoto wao ni kutowapa nafasi ya kushiriki michezo lakini pia kushindwa kufuatilia
taratibu za kuwapatia chanjo zinazohitajika kwa watoto kulingana na umri wao
“Chanjo ni mojawapo ya hatua bora zaidi za afya ya umma na kuokoa watoto wanaokadiriwa kuwa milioni mbili mpaka tatu kwa mwaka.
Hata hivyo, katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, viwango vya watoto wanaohudhuria kliniki kupata chanjo kimepungua, kwenye
tamasha hili tutawakumbusha wazazi juu ya haya yote,” alisema Dk Mahita
Alisema michezo mbalimbali itakuwepo kwa watoto kuanzia umri wa miaka 4 hadi 15 ambao watashiriki kucheza mpira wa miguu, riadha, kuogelea, kuvuta kamba na mengineyo.