MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amegawa majiko ya Gesi 162 kwa wajasiriamali wanawake wa Jimbo hilo ikiwa ni mpango wa serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan wa kuwawezesha akina mama kiuchumi.
Akikabidhi majiko hayo ,Mtaturu amesema wajasirimali hao wakitumia nishati mbadala hata biashara yao itakuwa nzuri na wataondokana na madhara yatokanayo na matumizi ya kuni ikiwemo uharibifu wa mazingira na madhara ya kiafya.
"Lengo la kutoa mitungi hiyo ya Gesi ni kuunga Kampeni ya kutumia Nishati mbadala na kuachana na matumizi Kuni na mkaa Ili kupambana uharibifu wa mazingira yetu na mabadiliko ya tabia nchi" alisema Mtaturu.
Tukio hilo limehudhuriwa na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ikungi wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mika Likapakapa ambaye amempongeza Mbunge Mtaturu kwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM kama alivyokabidhiwa wakati wa uchaguzi 2020.
"Mh Mtaturu amekuwa anachukua kero za wananchi kila mara na kuleta mrejesho wa miradi ya maendeleo kila mahali,".
"Pia, jambo la leo alilofanya la kuhamasisha utunzaji mazingira kupitia utumiaji wa nishati mbadala na kugawa mitungi ya gesi kwa makundi haya itakuwa chachu kubadilisha tabia ya kukata miti hovyo,"amesema Likapakapa.
Social Plugin