Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC MNDEME AKAGUA UJENZI WA SOKO KUU SHINYANGA..... "SIJAFURAHISHWA NA KASI YA UJENZI, NATAKA BIASHARA ZIANZE IFIKAPO OKTOBA 11"

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa tano kushoto) akikagua ujenzi wa Soko Kuu Mkoa wa Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo Jumatatu Septemba 11,2023 amekagua maendeleo ya Mradi wa Ukarabati wa Vibanda 106 vya biashara Soko Kuu Mkoa wa Shinyanga ambapo ameeleza Kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa soko hilo.

Ujenzi wa mradi wa Soko Mkuu Mjini Shinyanga ulianza Novemba 1,2022 na ulitarajiwa kukamilika Aprili 30,2023 lakini mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 57 hali iliyomfanya Mkuu huyo wa Mkoa kuagiza ujenzi huo ukamilike kufikia Oktoba 11,2023 sehemu ya chini ianze kutumika.

“Sijafurahishwa na kasi ya ujenzi wa mradi hu, haiwezekani tangu mwezi Aprili mpaka leo mradi huu mkubwa utakaogharimu shilingi Bilioni 1.8 haujakamilika. Nataka ifikapo Oktoba 11,2023 eneo la chini lianze kufanya kazi, tukamilishe ili kazi zingine ziendelee, msipokamilisha hatutaelewana. Lakini ifikapo Desemba 11,2023 huko juu pia tuwe tumekamilisha. Si Zaidi ya tarehe 11.12.2023 biashara ianze hapa”,amesema Mkuu wa Mkoa.

“Nataka biashara ianze kufanyika, wafanyabiashara hawa wakianza kazi mzunguko wa fedha utaongezeka”,ameongeza.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa amewataka wafanyabiashara waepuke kutumia watu wa kati (Madalali) ili kupata vibanda vya biashara huku akisisitiza kuwa serikali itachukua hatua kwa mtu yeyote atayeendekeza rushwa.

“Acheni kutumia madalali kupata vibanda, na anayepewa kibanda awe anafanya biashara. Vibanda hivi asiwepo mtu wa katikati (dalali), kama hujaridhika au kama kuna changamoto naomba tukae chini hadi tuelewane. Hakikisheni pia pesa zinalipwa halmashauri”,amesema Mhe. Mndeme.

Aidha ameagiza katika masoko yote patengewe eneo la faragha kwa ajili ya akina mama kunyonyesha watoto na kuchezea watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kushoto) akishiriki ujenzi wa Soko Kuu Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme  akikagua ujenzi wa Soko Kuu Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme  akikagua ujenzi wa Soko Kuu Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme  akizungumza katika Soko Kuu Mkoa wa Shinyanga
Wananchi na wafanyabiashara wakimshikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme  akizungumza katika Soko Kuu Mkoa wa Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme  akisikiliza na kujibu hoja/kero za wafanyabiashara katika Soko Kuu Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme  akiandika hoja/kero za wafanyabiashara katika Soko Kuu Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme  akiandika hoja/kero za wafanyabiashara katika Soko Kuu Mkoa wa Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com