Na Abel Paul, Jeshi la Polisi Dar es salaam.
Chama cha Ushirikka wa kuweka akiba na kukopa Usalama wa raia Saccos URA SACCOS ambacho kipo chini ya Jeshi la Polisi kimeendelea kuboresha mifumo ambapo chama hicho wamezindua mfumo wa URAMobile ambao utawasaidia wanachama kupata huduma masaa ishirini nane.
Akiongea leo Septemba 30,2023 wakati wa hafla ya uzinduzi mfumo huo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini amekipongeza chama hicho kwa namna ambavyo waendelea kutoa huduma bora kwa wanachama ambao ni askari na raia.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Sagini amepongeza chama hicho kwa namna ambavyo wametekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akisisitiza matumizi ya Tehama ndani ya Jeshi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura ameipongeza bodi ya URA Saccoss kwa kuendesha chama hicho kwa weledi mkubwa huku akimpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu IGP Saidi Mwema kwa ubunifu wake wa kuanzisha chama hicho ambacho kimeendelea kuweka ustawi bora kwa askari na raia ambao ni wanachama wa chama hicho.
Naye Kamishna wa Polisi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii CP Benedict Wakulyamba amesema chama hicho kimeendelea kukua kwa hisa ambapo amebainisha kuwa hisa hizo zimefika bilioni kumi na moja pointi tano nne bilioni (11.54) huku akiongeza kuwa kuwa chama hicho kimeendelea kukua ambapo idadi ya wanachama wanaokopa imeongezeka.