Hii ni mara ya tatu kwa Tanzania kufanya uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu.
Dkt. Biteko ambaye ni mbunge wa Bukombe, mkoani Geita atakuwa anashughulikia uratibu wa shughuli za Serikali.
Mwaka mmoja baada ya Rais Ali Hassan Mwinyi kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muhula wa kwanza wa miaka mitano Oktoba 1985, alimteua Salim Ahmed Salim kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Januari 24, 1993 Rais Mwinyi alimpandisha cheo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Augustine Mrema, kuwa Naibu Waziri Mkuu huku akiendelea kushikilia cheo chake cha Waziri wa Mambo ya Ndani.