Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ,Mhe. Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Chalinze.
NA ELISANTE KINDULU, CHALINZE
NAIBU Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Ridhiwani Kikwete, amewakumbusha waheshimiwa madiwani kuendelea kutatua changamoto za wananchi katika maeneo yao ya utawala.
Mhe. Ridhiwani aliyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani kilichoketi mwishoni mwa juma hili mjini Chalinze.
Mhe. Kikwete ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Chalinze amesisitiza kwamba ,changamoto zinazotakiwa kutatuliwa na madiwani ndani ya maeneo yao zisisubiri viongozi wa ngazi za juu kushughulikia.
Katika hatua nyingine, baraza la madiwani limemchagua kwa kishindo Mhe. Mawazo Ramadhani Mkufya kuwa makamu Mwenyekiti kwa kupata kura 19 Kati ya kura 21.
Kwa mujibu wa sheria ya Serikali ya Mitaa katika mamlaka za Wilaya, sura ya 287 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, baraza hilo limepata wenyeviti na wajumbe wa kamati mbalimbali.
Mh. Hassan Mwinyikondo kuiongoza kamati ya fedha, uongozi na mipango, Mhe. Mussa Gama kamati ya
uchumi ,ujenzi na mazingira, Mh. Selestine Semiono kamati ya Elimu, afya na maji, Mh.Mawazo R. Mkufya kamati kudhibiti UKIMWI, wakati kamati ya maadili ikiwa chini ya Mh. Mwanakesi Madega.
Nafasi ya Mwakilishi wa bodi ya ajira imeenda kwa Mhe. Mussa Gama. Huku Mwakilishi wa ALAT akiwa Mh. Mohamed Gelegeza pamoja na Mh. Anzali Ramadhani