Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari (katikati) akisaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9. Bw. Simon Masike alisaini kwa upande wa kampuni ya Indra Avitech. Hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imesaini kandarasi ya mfumo wa usimamizi wa taarifa za anga na Kampuni ya Indra Avitech kwa ajili ya kuboresha usalama wa safari angani katika anga ya Tanzania kupitia utoaji wa taarifa za anga zenye ubora wa hali ya juu, salama na muhimu kwa wakati sahihi kwa wadau mbalimbali wa usafiri wa anga.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari leo Mamlaka hiyo imesaini mkataba wenye thamani ya Shilingi Bilioni Tisa kwa ajili ya kubuni, kusambaza, kusanikisha, kuunganisha, na kuzindua Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Anga ambapo Mradi huu utatekelezwa kwa miezi 18.
Amesema sehemu ya mpango thabiti wa Usimamizi wa Taarifa za Anga (AIM) wa kuboresha mfumo wake wa taarifa za anga kwa kutoa usimamizi wa taarifa za anga kwa njia ya kisasa zaidi kwa kutoa na kubadilishana taarifa za anga za dijitali zenye ubora na kushirikiana na pande zote hivyo kuhakikisha usalama, utaratibu, na ufanisi wa urambazaji wa anga wa kitaifa na kimataifa.
“Lengo la utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Anga ni kuboresha mfumo wa AIM katika kuboresha usahihi wa data, upatikanaji, na ufanisi kwa kuzingatia mahitaji ya Upandishaji wa Mfumo wa Anga wa Usafiri (ASBU), na kufuata viwango vya kitaifa na kimataifa” ,Alisema Johari
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari (katikati), Mkurugenzi Huduma za Sheria TCAA, Maria Makala (wa pili kulia), Mwakilishi wa Kampuni ya Indra Avitech , Bw. Simon Masike(wa pili kushoto) wakisani Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023.
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari (wa pili kushoto) akikabidhiana mkataba na Mwakilishi wa Kampuni ya Indra Avitech, Bw. Simon Masike mara baada ya kusaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023. Mkurugenzi Huduma za Sheria TCAA, Maria Makala (wa pili kulia).
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari (katikati) pamoja na Mwakilishi wa Kampuni ya Indra Avitech, Bw. Simon Masike ( wa pili kushoto) wakionesha mkataba mara baada ya kusaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023.Wa pili kulia ni Mkurugenzi Huduma za Sheria TCAA, Maria Makala
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari (katikati) akizungumza wakati wa kusaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023.
Mwakilishi wa Kampuni ya Indra Avitech, Bw. Simon Masike akizungumza wakati Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) waliposaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023.
Kaimu Mkurugenzi Wa Huduma Za Uongozaji Ndege TCAA, Hamis Kisesa akizungumza wakati Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) waliposaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga na Kampuni ya Indra Avitech wenye thamani ya Tsh. Bilioni 9 iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA Septemba 22, 2023.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA,Bw. Daniel Malanga(katikati), Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Bw. Teophory Mbilinyi (kushoto) na Mkurugenzi Huduma za Sheria TCAA, Maria Makala wakiwa kwenye hafla ya kusaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano TCAA, Yessaya Mwakifulefule(kushoto), Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kinachomilikiwa na TCAA, Aristid Kanje (katikati) na Afisa Mtoa Taarifa za Anga Mwandamizi (TCAA) wakiwa kwenye hafla ya kusaini Kandarasi ya Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa uSafiri wa anga wakiwa kwenye hafla ya kusaini Kandarasi ya Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Utoaji wa Taarifa za Anga.
Picha za pamoja