SERIKALI YAPANGA KUNUNUA MITAMBO 15 YA UCHORONGAJI MIAMBA



Oktoba 2023 mitambo mitano itatolewa mkoani Dodoma

• Sekta inachangia 56 % ya fedha za kigeni

Serikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya uchorongaji wa miamba kwa ajili ya utafiti wa kina wa Madini.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 25 , 2023 na Waziri wa Madini Mhe. Mavunde wakati akiongea katika kipindi cha Jambo Tanzania (TBC1) kutokea  viwanja vya maonesho vya  EPZ bomba mbili mkoani Geita. 

Akielezea kuhusu mkakati wa  VISION 2030 Madini ni Maisha na Utajiri Mhe. Mavunde  amesema kuwa Serikali imejipanga kufanya utafiti wa Madini nchi nzima kwa lengo la kupata taarifa zitakazo weza kufungamanisha sekta ya Madini na Sekta nyingine za kiuchumi.

Akifafanua hali ya utafiti wa Madini  amesema mpaka sasa utafiti wa kina umefanyika kwa asilimia 16 tu ambazo taarifa zake ndio zinatumika lengo  la Serikali ni kuongeza taarifa kupitia tafiti nyingine ziitakazofanywa na GST.

Mpaka sasa Sekta ya Madini inachangia asilimia 56 ya Fedha za kigeni ambazo zinachangia asilimia 9.1 ya pato la Taifa(GDP) , hii ni kwa utafiti wa 16% uliofanyika , hivyo kufikia 2030 tutakuwa  tumefanya utafiti nchi nzima.

Sambamba na hapo Mhe. Mavunde ameeleza kuwa Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira  zitaendeleza juhudi za kutunza mazingira kama Sheria zinavyoelekeza.

Pia Mhe. Waziri Mavunde ameshiriki zoezi la upandaji miti katika viwanja vya maonesho vya EPZ.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post