Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa Bupe Mwakang'ata ameshiriki Kampeni ya kumuombea kura Mgombea wa Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Mbarali Bahati Ndingo katika kata ya Mawindi Mkoani Mbeya
Akizungumza leo katika Kata hiyo Mhe. Bupe amewasii wananchi wa Kata ya Mawindi kutofanya makosa ifikapo tarehe 19/9/2023 kumpa kura nyingi Bahati Ndingo kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali .
“Mlifanya uamuzi mzuri wa kumpitisha Bahati Ndingo kuwa Mgombea wa jimbo hili,sisi kama wabunge wanawake tunaotoka katika Jumuiya ya UWT tumekuja hapa kuhakikisha Ndugu Bahati anashinda kwa kishindo kupitia chama chetu cha CCM”,amesema.
Social Plugin