Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetambulisha na kuzindua Programu Shirikishi ya Kupinga Ndoa za Utotoni wenye lengo la kuondoa aina zote za ukatili wa kijinsia katika jamii ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mradi huo umetambulishwa leo Jumatatu Septemba 4,2023 wakati wa kikao cha majadiliano kuhusu masuala ukatili wa kijinsia kilichokutanisha wadau mbalimbali katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga uliopo Iselamagazi.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, ameishukuru Tume ya Taifa ya UNESCO kwa kuleta mradi ambao amesema utakuwa chachu ya mapambano dhidi ya ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia.
Ngwale amesema mradi huo umekuja wakati ambapo mkoa wa Shinyanga uko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto na umekuwa wa kwanza kwa Tanzania bara kuwa na Mpango Mkakati wa kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia (2020-2025) unaozingatia vipaumbele vya mkoa kwa kushirikiana na wadau huku akibainisha kuwa endapo utafiti mpya utafanyika anaamini hali ya ukatili itakuwa imeshuka katika mkoa wa Shinyanga ikilinganishwa na miaka ya nyuma na utakuwa mkoa wa mfano wa kuja kujifunza kwa mikoa mingine.
“Jamii bado inakabiliwa na tatizo la ndoa za utotoni na vitendo vya ukatili wa kijinsia,tunaamini mradi huu ambao unaunga juhudi za serikali katika kutokomeza ukatili wa aina zote ndani ya jamii utakuwa chachu kubwa ya kuleta mabadiliko kwani tunataka watoto wetu wawe salama ili waweze kutimiza ndoto zao”,amesema Ngwale.
Amesema ili kutokomeza ukatili wa kijinsia ni lazima kila mmoja awajibike katika kupaza sauti hasa katika kipindi hiki ambacho watoto wanakabiliwa na changamoto na vitendo viovu vinavyosababishwa na mmomonyoko wa maadili ikiwemo ubakaji na ulawiti.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Aboud Khamis amepongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassa kwa namna anavyosimamia masuala ya usawa wa kijinsia huku akiitaka Jamii kuanzia ngazi ya familia kuwajibika kupinga ndoa za utotoni kwa kuanza kuwafundisha watoto wa kike na wa kiume madhara ya ndoa za utotoni na kukemea ndoa hizo katika jamii.
“Tanzania kama nchi inayoendelea inakabiliwa na changamoto kadhaa za kijamii kama vile kukosekana kwa usawa wa kijinsia katika baadhi ya masuala katika jamii zetu. Suala hili linapelekea kuibuka kwa changamoto zingine katika jamii hususani ndoa za utotoni",amesema.
Ameongeza kuwa, Ndoa za utotoni zina athari kubwa sana katika ukuaji wa mtoto wa kike ikiwa ni pamoja na kushindwa kupata haki zake za msingi (kukosa Elimu, kushindwa kufikia ndoto yake, kupitia manyanyaso yanayoleta maumivu ya kimwili na kihisia, na kuwa katika hatari ya kupoteza maisha wakati wa ujauzito au kujifungua.)
“Ili kuhakikisha kuwa usawa wa kijinsia katika nchi yetu, Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuko hapa kwa ajili ya kujenga uelewa wa pamoja na program endelevu ya kupinga ndoa za utotoni ili kumlinda mtoto wa kike na kuchochea maendeleo ya Jamii na Taifa kwa ujumla”,ameongeza Khamis.
Katika hatua nyingine amesema katika kuhakikisha Dunia inakuwa mahali salama pa kuishi Sekta ya Sayansi Jamii ya tume hiyo, wanatekeleza lengo namba tano la malengo endelevu kwa kufanya na kusimamia Masuala ya Vijana, Usawa wa Kijinsia, Kupinga matumizi haramu ya madawa katika michezo, Usimamizi wa masuala ya mabadiliko ya kijamii na Taaluma ya maadili katika utabibu.
Mshauri Mwelekezi wa Mradi wa Kupinga Ndoa za Utotoni unaotekelezwa na Tume ya Taifa ya UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Dkt. Rehema Horera John ameitaka jamii kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara ya ndoa za utotoni, kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake, atekeleze wajibu wake kwani Ndoa za utotoni ukatili wa kijinsia vinazuilika.
Mshauri Mwelekezi wa Mradi wa Kupinga Ndoa za Utotoni unaotekelezwa na Tume ya Taifa ya UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la UNESCO Dkt. Rehema Horera John.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga, Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Joseph Ntomela amesema mradi huo utasaidia kuiongezea nguvu serikali katika kukomesha ndoa za utotoni hivyo kutimiza ndoto za watoto ambao ndoto zao zimekuwa zikikatishwa.
Afisa Programu Mkuu Sayansi ya Jamii kutoka Tume ya Taifa ya UNESCO, Bi. Uyanjo Lazarus amesema mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika kata za Iselamagazi, Ilola na Lyabusalu ambapo umelenga kuelimisha jamii juu ya athari za ukatili wa kijinsia na ndoa za utotoni, kuwawezesha wanajamii hususani viongozi katika ngazi zote kuendelea kupiga vita ukatili wa kijinsia na ndoa za utotoni lakini pia kuhamasisha jamii, vijana na mabinti juu ya thamani na haki yam toto wa kike na kiume ya kukua na kuishi katika mazingira salama ili aweze kutimiza ndoto yake.
Nao washiriki wa kikao hicho wameeleza kukerwa na baadhi ya viongozi wenye dhamana wakiwemo viongozi wa dini, siasa ambao wamekuwa wakishiriki katika ndoa za watoto hivyo kukwamisha mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakati Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikitambulisha Programu Shirikishi ya Kupinga Ndoa za Utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakati Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikitambulisha Programu Shirikishi ya Kupinga Ndoa za Utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Aboud Khamis akizungumza kwenye kikao cha kutambulisha Programu Shirikishi ya Kupinga Ndoa za Utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Afisa Programu Mkuu Sayansi ya Jamii kutoka Tume ya Taifa ya UNESCO, Bi. Uyanjo Lazarus akizungumza kwenye kikao cha kutambulisha Programu Shirikishi ya Kupinga Ndoa za Utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Aboud Khamis na Afisa Programu Mkuu Sayansi ya Jamii kutoka Tume ya Taifa ya UNESCO, Bi. Uyanjo Lazarus (kushoto) wakijitambulisha kwenye kikao cha kutambulisha Programu Shirikishi ya Kupinga Ndoa za Utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa MTAKUWWA Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Aisha Omary akizungumza kwenye kikao cha kutambulisha Programu Shirikishi ya Kupinga Ndoa za Utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Joseph Ntomela akizungumza kwenye kikao cha kutambulisha Programu Shirikishi ya Kupinga Ndoa za Utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mshauri Mwelekezi wa Mradi wa Kupinga Ndoa za Utotoni unaotekelezwa na Tume ya Taifa ya UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la UNESCO Dkt. Rehema Horera John akiwasilisha mada kuhusu masuala ya Ukatili wa Kijinsia

Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE, John Myola akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Mchungaji Samuel Mabula Kulwa kutoka kata ya Lyabusalu akichangia hoja kwenye kikao hicho
Afisa Programu Mkuu Sayansi ya Jamii kutoka Tume ya Taifa ya UNESCO, Bi. Uyanjo Lazarus akizungumza na waandishi wa habari
Afisa Programu Mkuu Sayansi ya Jamii kutoka Tume ya Taifa ya UNESCO, Goodluck Patrice akizungumza wakati wa kikao hicho
Kikao cha kutambulisha Programu Shirikishi ya Kupinga Ndoa za Utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kikiendelea

Kazi za vikundi zikiendelea wakati wa kikao cha kutambulisha Programu Shirikishi ya Kupinga Ndoa za Utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga

Viongozi wa kutoka Tume ya Taifa ya UNESCO wakipiga picha ya kumbukumbu na Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale (wa pili kushoto mbele) aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga na Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Joseph Ntomela aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga ( wa kwanza kulia mbele)

Washiriki wa kikao cha kutambulisha Programu Shirikishi ya Kupinga Ndoa za Utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu

Washiriki wa kikao cha kutambulisha Programu Shirikishi ya Kupinga Ndoa za Utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Soma pia
Social Plugin