SERIKALI YAANZA MPANGO WA UNUNUZI WA DHAHABU


•Yapanga kununua Tani 6

•TRA watoe elimu kuhusu kodi ya 2%

**
Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imeanza mpango maalum wa ununuzi wa Madini ya dhahabu kwa lengo la kuongeza akiba ya nchi ya fedha za kigeni.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wakati akifungua Maonesho ya Sita (6) ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Dkt.Biteko aliipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa kuanza mpango wa ununuzi wa Madini ya dhahabu na kuhifadhi ambapo mpaka sasa BoT imenunua kiasi cha kilogram 418 za dhahabu yenye kiwango cha asilimia 99.9. 

Akizungumza kuhusu mpango huo Dkt.Biteko alisema kuwa BoT imepanga kununua kiasi cha Tani sita kutoka kwa wachimbaji na wauzaji wa Madini nchini.

Vilevile kuhusu maendeleo ya Sekta Madini, alisema uwepo wa viwanda vizuri vyenye teknolojia ya kisasa katika uchakataji  na usafishaji wa madini ya dhahabu ndani ya nchi  kumepelekea kujenga imani kwa wanunuzi mbalimbali akiwemo  BoT tofauti na awali kabla ya kuwepo kwa viwanda uchakataji na usafishaji kufikia kiwango cha asilimia 99.9.

Akielezea juu ya mpango huo Dkt. Biteko alielekeza kuwa ni vyema kuwepo na mkakati mzuri wa kuwafiki wachimbaji wadogo popote watakapo chimba ili wauze dhahabu kwa uwazi na bei itakayoendana na soko la Dunia kukifanyika hivyo kutaondoa mawazo ya  utorosha wa Madini.

Pia ameelekeza kuundwa Kanuni mpya za uchenjuaji Madini ili wachenjuaji waweze kufanya kazi zao kwa imani na uhakika kwa kufuata hizo kanuni zitakazo undwa.

Akizungumza kuhusu Vision 2030 ni Maisha na Utajiri , Dkt. Biteko alisema kuwa mpango wa Serikali ni kuwa ifikapo 2025 sekta ya Madini ichangie asilimia 10 katika pato la taifa hivyo juhudi zifanyike katika ukusanya mapato.

Sambamba na hapo aliwaelekeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo wa Madini juu ya malipo ya asilimia mbili (2%) kwa wachimbaji wadogo katika uzalishaji wao ili wapate elimu hiyo na kuona umuhimu wa kulipa kodi husika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post