Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wakili Stephen Byabato, Jana 23 Septemba, 2023 ameshiriki zoezi la usimikaji wa Bendera za Chama Cha Mapinduzi CCM na kusalimia mabalozi ambapo zoezi hilo linaendelea kwenye kata zote kumi na nne (14) za Jimbo la Bukoba Mjini, na jana ilikuwa zamu ya kata ya Kahororo.
Pia zoezi hilo limeudhuriwa na wanachama wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kahororo pamoja na kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Bukoba Mjini, Umoja wa vijana Ccm wilaya (UVCCM).
Pamoja na usimikaji wa Bendela Mheshimiwa Byabato amezungumza na wananchi wa kata ya Kahororo kwa kusikiliza kero zinazowakabili ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Social Plugin