ZAIDI YA WATU 2,000 WAMERIPOTIWA KUNG’ATWA NA MBWA




KAIMU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw.Arbogast Warioba,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa yaliyofanyika leo Septemba 28,2023 wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Na DOTTO KWILASA, DODOMA

Dunia ikiwa inaadhimisha siku ya kichaa cha mbwa,zaidi ya watu 20,000 wameripotiwa kung’atwa na mbwa kwa kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka huu hapa nchini huku mkoa wa Dar es Salaam ukiwa unaongoza kuwa na idadi nyingi ukifuatiwa na mikoa ya Dodoma , Morogoro na Arusha.

Akizungumza leo Sept 28,2023 wakati wa siku ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa duniani iliyofanyika katika wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Arbogast Warioba amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti 201,2023 jumla ya watu 20,005 walitolewa taarifa ya kung’atwa na Wanyama.

Amesema kutokana na hali hiyo Serikali imechukua hatua za kuudhibiti ugonjwa huo kwa kutoa jumla ya dozi 180,000 za chanjo ambazo tayari zimesambazwa katika halmashauri 26 nchini kuanzia septemba mwaka huu ambapo jumla ya mbwa 20,426 na paka 740 wameshakuchanjwa.

Ametaja mikoa minne inayoongoza kuwa na matukio ya kung’atwa na Wanyama ni Dar es Salaam, matukio 3,321, Dodoma matukio 3,136,Morogoro matukio 1,559, na Arusha matukio 1,155 na takwimu hizo zinajumuisha wananchi waliopata huduma katika vituo vya afya.

Pia amesema ugonjwa wa kichaa cha mbwa unakadiriwa kusababisha takribani vifo 59,000 kwa mwaka duniani, ambapo asilimia 36 ya vifo hivyo hutokea katika bara la Afrika, pia asilimia 30 hadi 50 ya waathirika wa ugonjwa huo ni watoto chini ya miaka 15 kwasababu ndio huwa karibu na mbwa wanaofugwa kwa muda mwingi, pia hupenda kucheza,kuchokoza mbwa wasiomfahamu njiani.

“Vimelea vya ugonjwa wa kichaa cha mbwa vinapoingia katika jeraha hushambulia mfumo wa fahamu kuanzia katika eneo la jeraha, kuelekea katika uti wa mgongo na hatimaye kuathiri mfumowa kati ya fahamu (ubongo)” amesema

Pamoja na hayo ameeleza kuwa katika juhudi za kudhibiti ugonjwa huo Serikali imeendelea kutoa elimu kwa umma, kuboresha utekelezaji way a afya moja nchini, kurahisisha upatikanaji wa huduma za chanjo ya kichaa cha mbwa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma ya chanjo kwa Wanyama hasa mbwa na paka.

Amesema Serikali imeshiriki katika michakato ya kidunia ambayo imewezesha mwaka huu 2023 Shirika la Usambazaji Chanjo Duniani (GAVI) kuridhia chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kichaa cha mbwa (Anti -rabies) kuingizwa katika mfumo wa chanjo za kawaida ambapo gharama zinatarajiwa kushuka zaidi pale taratibu za utekelezaji wa jambo hilo utakapokamilika.

Kawa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa afya ya mifugo ngazi ya jamii Stanford Ntabalema ameeleza kuwa ugonjwa huo huishi kwenye baadhi ya Wanyama wa porini ikiwemo popo ambapo husambaa kupitia Wanyama wa nyumbani kwa kuambukizwa.

“Mbwa na Wanyama wengine wenye virusi vinavyosababisha kichaa cha mbwa huweza kuambukiza bila kuonesha dalilizozote,hivyo ni muhimu mtu yeyote aking’atwa na mbwa au mnyama mwingine atoe taarifa kwa mtaalamu wa mifugo ili hatua husika zichukuliwe,”alisema

Naye, mwakilishi wa wizara ya Afya Dk.Robert Kishimba amesema ugonjwa huo ni hatari na hautibiki ambapo kati ya watu 1000 wanaong'atwa na mbwa ni mmoja tu anayeweza kupona hivyo ni lazima kuuepuka kwa kuwakinga Wanyama kama mbwa,paka na wengine .

Aidha jamii inapaswa kuepuka tabia hatarishi za kumchokoza mbwa au kumpiga ikiwa ni pamoja na kuelimisha watoto wwasicheze na mbwa wasiyemfahamu.

Naye mtaalamu wa magonjwa ya mbwa Ofisa mifugo wilaya ya Kongwa Dk.Kisimba Benjamin ameeleza kuwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa huanza kipindi cha baridi ambapo dalili zake ni mbwa kutoa ute usioisha,mbwa kung’ata vitu ovyo,kuogopa maji,kubadili tabia na kupoteza fahamu .


KAIMU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw.Arbogast Warioba,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa yaliyofanyika leo Septemba 28,2023 wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.


Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Bi.Irene Milinga,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa yaliyofanyika leo Septemba 28,2023 wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.


Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw.Arbogast Warioba (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa yaliyofanyika leo Septemba 28,2023 wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.


Mwakilishi wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Gerald William,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa yaliyofanyika leo Septemba 28,2023 wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.


MWAKILISHI wa Mkurugenzi wa huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt.Rogath Kishimba,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa yaliyofanyika leo Septemba 28,2023 wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi Afya ya Jamii ya Veterinari Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt.Stanford Ndibalema,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa yaliyofanyika leo Septemba 28,2023 wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,bunge na Uratibu Luteni Kanali Selestinr Masalamando,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa yaliyofanyika leo Septemba 28,2023 wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.


KAIMU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw.Arbogast Warioba,akiangalia Mbwa wakipata chanjo ya Kichaa cha Mbwa wakati wa maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa yaliyofanyika leo Septemba 28,2023 wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.



Wananachi mbalimbali wakiwa wamewaleta Mbwa kupata chanjo ya Kichaa cha Mbwa wakati wa maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa yaliyofanyika leo Septemba 28,2023 wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.


KAIMU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw.Arbogast Warioba,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhutubia maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa yaliyofanyika leo Septemba 28,2023 wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post