CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAA (DMI) CHAZINDUA DAWATI LA JINSIA


Makamu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Fedha Utawala na Mipango, Dkt. Lucas Mwisila akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Dawati la Jonsia katika Chuo hicho. Hafla hiyo imefanyika Septemba 8, 2023. Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Dawati la Jinsia vyuo vikuu na vyuo vya kati kutoka wizara ya maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na makurdi maalum, Gift sowoya akizungumza katika hafla hiyo

Mkuu wa Kituo cha Polisi Buguruni OCS Sarah Bundara akizungumzia uwepo wa madawati ya Jinsia chini kulivyoleta matokeo chaya kupambana na ukatili wa kijinsia.

Picha ya pamoja

(PICHA NA: HUGHES DUGILO) Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

Chuo cha Bahari Dar es Salaam, (DMI), kimezindua Dawati la Kijinsia litalojihusisha kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi na watumishi katika chuo hicho.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Dawati hilo, Makamu Mkuu wa Chuo cha DMI, Fedha Utawala na Mipango, Dkt. Lucas Mwisila amesema uwepo wa Dawati hilo ni hatuna kubwa iliyofikiwa na Chuo hicho katika kuhakikisha changamoto za ukatili wa Kijinsia chuoni hapo zinashughulikiwa.

Ameeleza kuwa matukio ya ukatili wa kijinsia yamekuwa yakiathiri vijana wengi kwenye jamii, na kwamba kwa mwanafunzi inaweza kumuathiri katika shughuli zake za kitaaluma.

Dkt. Mwisila ameyasema hayo Septemba 8, 2023 Jijini Dar es Salaam, katika hafla fupi ya uzinduzi wa Jukwaa la Kiijinsia lenye lengo la kupambana na ukatili wa Kiijinsia kwa wanafunzi, walimu na watumishi waliopo katika hicho.

Kwa upande wake mratibu wa Dawati la Jinsia vyuo vikuu na vyuo vya kati kutoka wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makurdi maalum, Bi. Gift sowoya, amesema kuwa kuanzishwa kwa Dawati hilo katika chuo hicho, kunaongeza idadi ya Madawati ya Kiijinsia kufikia 421 katika Taasisi mbalimbali za Elimu hapa nchini.

“Niwapongeze Chuo cha DMI kwani wamekuwa miongoni mwa Taasisi zilizotekeleza mwongozo huu, kwani mpaka sasa tuna Madawati 420, na hili tuliloanzisha leo hapa DMI tumefikia Madawati 421.

“Dawati hili halipo tu kwa wanafunzi peke yao, bali litashughulika na watu wote wanaofanyakazi katika chuo hiki wakiwepo walimu. Naomba wote mlitumie bila kubagua” amesema Sowoya.

Naye, Mkuu wa Kituo cha Polisi Buguruni OCS Sarah Bundara amsema uwepo wa Madawati ya Jinsia kumesaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na ukatili wa kijinsia ukizingatia tatizo hilo limekuwa kubwa kwenye jamii, kutokana na uwepo wa watoto wa kiume kuhusishwa na vitendo hivyo.

“Tumekuwa tukipokea kesi nyingi za ukatili kwa watoto na watu wazima pia, kesi hizi zipo, na sasa hata watoto wa kiume wameingia kwenye changamoto hiyo.

“Watoto wa kiume nao wanahitaji kulindwa kama ilivyo kwa watoto wa kike, kwa sababu mazingira na mabadiliko ya teknolojia imepelekea kuingia katika ukatili bila wao mwenyewe kujua” amesema OCS Bundara.

Ameeleza kuwa katika madawati yao wamekuwa wakipokea kesi za uwepo wa rushwa ya ngono vyuoni kutokana na sababu mbalimbali, ambapo amekipongeza Chuo cha DMI kuanzisha Dawati hilo litalowafikia wanafunzi kueleza vitendo vya ukatili wa kijinsi wanavyokabiliana navyo ikiwemo vitendo vya rushwa ya ngono.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post