Jeshi la Polisi Mkoa wa
Morogoro linamsaka dereva wa basi la Abood lenye namba za Usajili T904 DKY
inayofanya safari zake za Dar es salaam na Tabora baada ya kusababisha ajali
kwa kuigonga gari aina ya Noah yenye namba za usajili T828 DNB asubuhi ya leo Septemba
11,2023.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwakwe
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Alex Mkama amesema ajali hiyo imetokea
katika eneo la Kitugwa Manispaa ya Morogoro ambapo katika ajali hiyo watu
wawili wamepoteza maisha huku majeruhi wawili wakiendelea kupatiwa matibabu
katika hospital ya Mkoa wa Morogoro.
Aidha Kamanda Mkama amesema kuwa chanzo cha ajali
hiyo ni dereva wa wa basi la Abood kutumia vibaya barabara jambo lililopelekea
kugongana na Noah iliyokuwa ikitokea Morogoro kuelekea Dar es salaam.
Kwa upande wake kaimu afisa Mahusiano wa Hospital
ya Mkoa wa Morogoro Scholastic Ndunga amesema kuwa wamepokea Maiti mbili na
majeruhi wawili ambao wametokana na ajali hiyo, japo taarifa za awali kutoka
kwa Kamanda Mkama zilieleza kuwepo na kifo kimoja na majeruhi watatu.
Social Plugin