Na. WAF, Mtwara
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu Septemba 13, 2023 ametembelea Hopsitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula na kukagua miradi ya jengo jipya la upasuaji, jengo jipya la wagonjwa wa nje (OPD), Jengo jipya la Wagonjwa wa dharura (EMD) pamoja na Jengo la wazazi (martenity) ambayo ipo katika hatua za mwisho za ukamilikaji.
Dkt.Jingu amesema kuwa lengo la Kufanya Ukaguzi Wa Miradi mbali mbali ya uboreshaji wa Huduma za Afya inayoendelea ni kuangalia ubora wa miradi hiyo kuendanda na thamani ya fedha iliyowekezwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili wananchi waweze kupata Huduma bora za afya.
Aidha Dkt. Jingu amepata wasaa wa kuzungumza na Watumishi wa Afya katika Hospitali hiyo na kuweza kusikiliza na kutatua baadhi ya changamoto wanazopitia watumishi hao.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara-Ligula, Dkt. Lobikieki Kissambu amemshukuru Dkt. Jingu kwa kuweza kutembelea Hospitali hiyo kwani ni faraja kwa uongozi na Watumishi kwa ujumla kutembelewa na wasimamizi kutoka ngazi ya juu.
Social Plugin