Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la usimamizi wa mazingira na maendeleo (EMEDO) Edwin Soko akielezea sababu za EMEDO kuwakutanisha waandishi wa habari katika warsha ya siku moja.
***
Na Tonny Alphonce,Dodoma
Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la usimamizi wa mazingira na maendeleo (EMEDO) Edwin Soko amewataka waandishi wa habari kuandika habari zinazotoa majibu ya migogoro au majanga yaliyopo badala ya uandishi usiotoa majawabu ya changamoto zilizopo katika jamii.
Soko ameyasema hayo leo tarehe 06/09/2023 mkoani Dodoma wakati akifungua warsha ya siku moja iliyofanyika jijini Dodoma iliyowakutanisha waandishi wa habari za Uvuvi kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwafahamisha wanahabari hao kuhusu mtandao wa kitaifa wa kuzuia kuzama na mradi wa kuzuia kuzama kwa maji na mradi wa kuzuia kuzama kwa ziwa Victoria.
Soko amesema ni muhimu kwa waandishi wa habari kubobea katika uandishi wa eneo moja kwa sababu mwandishi anaweza kuandika habari kwa kina ambayo inaweza kuleta mabadiliko katika jamii na taifa kwa ujumla.
Akizungumzia mradi wa kuzuia kuzama maji unaotekelezwa na EMEDO,Soko amesema kwa waandishi ni muhimu kushiriki kwa kuandika habari za kuujulisha Umma umuhimu wa kuchukua tahadhari wanapokuwa majini.
Mwanahabari Sudi Shaaban akijitambusha katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na shirika la EMEDO kwa lengo la kuwafahamisha wanahabari juu ya Mtandao wa Kimataifa wa kuzuia kuzama maji Tanzania pamoja na mradi wa kuzuia kuzama katika ziwa Victoria unaotekelzwa na EMEDO.
Mwandishi wa habari Georgi Binagi akijitambusha katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na shirika la EMEDO kwa lengo la kuwafahamisha wanahabari juu ya Mtandao wa Kimataifa wa kuzuia kuzama maji Tanzania pamoja na mradi wa kuzuia kuzama katika ziwa Victoria unaotekelzwa na EMEDO.
Mwandishi wa habari Glory Kiwia akijitambusha katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na shirika la EMEDO kwa lengo la kuwafahamisha wanahabari juu ya Mtandao wa Kimataifa wa kuzuia kuzama maji Tanzania pamoja na mradi wa kuzuia kuzama katika ziwa Victoria unaotekelzwa na EMEDO.
Mwandishi James Lerombo akijitambusha katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na shirika la EMEDO kwa lengo la kuwafahamisha wanahabari juu ya Mtandao wa Kimataifa wa kuzuia kuzama maji Tanzania pamoja na mradi wa kuzuia kuzama katika ziwa Victoria unaotekelzwa na EMEDO.
Meneja Mradi wa kuzuia kuzama maji Arthur Mugema kutoka shirika la EMEDO akizungumzia namna mradi unavyotekelezwa katika ziwa Victoria.
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia kikao cha siku moja kilichoandaliwa na shirika la EMEDO kwa lengo la kuwafahamisha wanahabari juu ya Mtandao wa Kimataifa wa kuzuia kuzama maji Tanzania pamoja na mradi wa kuzuia kuzama katika ziwa Victoria unaotekelzwa na EMEDO.