Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Dkt Yose Mlyambina akihutubia wakati wa uapisho wa Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) katika ukumbi wa Mahakama ya kazi Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Mhe. Usekelege Mpulla akila kiapo mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Dkt Yose Mlyambina wakati wa uapisho huo uliofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Kazi Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Mhe. Usekelege Mpulla akitoa shukrani mara baada ya uapisho uliofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Kazi Jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa Taasisi na Vitengo ambavyo vipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakimsikiliza Mhe Jaji alipokuwa akihutubia wakati wa uapisho wa Mkurugenzi wa CMA uliofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Kazi jana Septemba 27,2023 Jijini Dar es Salaam.
.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Dkt Yose Mlyambina amewataka watumishi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kutumikia jamii ya Tanzania kwa uaminifu na haki wakati wa utatuzi wa migogoro ya kikazi.
Aidha, amesema wanapaswa kuwa watu wenye hekima pindi wanapotekeleza majukumu ya Tume, kufanya hivyo wataongeza imani kwa wananchi.
Ameyasema hayo Septemba 27, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa Uapisho wa Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) iliyofanyika katika Ukumbi wa Mahakama ya Kazi.
Sambamba na hayo, Dkt. Mlyambina amesema Watumishi wa Tume pamoja na Mahakama wana wajibu mkubwa wa kuelimisha jamii kuhusu usuluhishi na kuhakikisha kuwa mashauri mengi yanatatuliwa kwa njia ya usuluhishi.
Naye, Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Mhe. Usekelege Mpulla ameishukuru Bodi ya Tume, Menejimenti pamoja na Watumishi, amehaidi kushirikiana nao katika utekelezaji wa majukumu ya Tume.
Vilevile, Mhe. Mpulla amesema migogoro inayohusu wafanyakazi na waajiri inapaswa kufanyiwa kazi haraka na kwa wakati ili kukuza uchumi wa Nchi.
Social Plugin