JAMII YATAKIWA KULINDA AMANI KWA KUEPUKA MATUMIZI HOLELA YA SILAHA

 


Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Mkuu wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania,Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Eva Stesheni amewataka wananchi kuchukua hatua dhidi ya silaha zinazozagaa mitaani na kutumika kinyume na taratibu ili kuweiweka jamii salama.

Ameeleza hayo wakati akitoa mada  ya madhara ya uzagaaji wa silaha ndogo na nyepesi kwa jamii wakati wa kikao cha Mtandao wa Polisi wanawake Tanzania  na viongozi wa makundi ya wanawake Mkoa wa Dodoma.

Alisema,wameamua kuwatumia wanawake Katika mapambano hayo Kwa kuwa ni Mashujaa wa ulinzi na amani kwenye jamii na kwamba Kila mwanamke akisimama kwenye nafasi yake hakuna silaha yoyote itazagaa mitaani bila utaratibu.

alisema kuwa madhara ya uzagaaji wa silaha ni makubwa kwenye jamii na hivyo ni wajibu wa kila mwanajamii kuwafichua wanaomiliki silaha kinyume cha utaratibu kuzisalimisha.

"Silaha zina madhara yake zikizagaa mitaani,wanaotumia silaha hizo  tunawaona kila leo na wengine tunawajua tunapaswa kuwafichua acheni kuwatunzia siri,” alisema

Naye Mkuu wa kitengo cha udhibiti na usajili wa silaha Kamishna Msaidizi wa Polisi,  Bertha Neema Mlay amesema kuwa katika my jitihada hizo watuhumiwa 220 walikamatwa kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria .

Aidha watuhumiwa 17 walikamatwa kwa kumiliki risasi kinyume cha sheria na kusisitiza kuwa juhudi bado zinaendelea.

“Mwaka jana 2022 baada ya mwezi Septemba jumla ya watuhumiwa 220 walikamatwa kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria na watuhumiwa 17 walikamatwa kwa kumiliki risasi kinyume cha sheria,” alisema


 Alisema kila mwaka Septemba huwa ni mwezi wa msamaha wa kusalimisha silaha zinazomilikiwa jkinyume cha sheria na baada ya Septemba huanza kuwakamata wanaomiliki silaha hizo kinyume cha sheria.

Alisema kuwa zoezi hilo lilitakiwa kukamilika Septemba 30, lakini limeongezewa muda hadi Oktoba 31,mwaka huu .

Alisema kuwa silaha ina faida ikitumika vyema kwa kazi iliyokusudiwa na wakati muafaka ila zikitumika kiholela na kinyume na ilivyokusudiwa inaleta madhara.

Pia sheria ya udhibiti na usajili wa silaha yam waka 2015 na kanuni zake za mwaka 2016 zinaruhusu mtu binafsi, kampuni kumilikishwa silaha, matumizi yaliyoainishwa kwenye sheria hiyo ni kujilinda binafsi, kulinda mazao na kulinda Wanyama, mashindano ya kulenga shabaha.

Amesema silaha inayomilikiwa kinyume na sheria ni silaha haramu.

Alisema kuwa madhara ya uzagaaji wa silaha ni kuongeza uhalifu migogoro, matishio, vita vya wenyewe kwa wenyewe na  kurudisha nyuma maendeleo.

Pia huleta ukatili wa kijinsia, kubaka, kulawiti, kilema cha kudumu, kuzorota kiuchumi.

"Kila ifikapo Novemba mosi wataanza kuwakamatawote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria,"amesisitiza .

Akizungumza kwenye mkutano huo, mmoja wa viongozi wanawake kutoka soko la Sabasaba.

Anna James,alitaka mabalozi kuwa na utaratibu wa kuwatambua watu wanaoingia kwenye maeneo yao ili kupunguza uhalifu.

“ Kuna maeneo ukienda lazima mwenyeji atoe taarifa kwa balozi wa nyumba 10, jambo hilo husaidia kujua pale uharifu unapotokea,” alisema

 “Kama maadili yameharibika hata wanawake wengi wanauawa kwa kutumia silaha.

Pia alitaka kuangaliwa kwa kisu kama silaha hatari kwa Maisha ya binadamu kwani kimekuwa kikitumika kufanya mauaji katika  matukio mengi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post