Inawezekana ukafikiria kuwa ni jambo la ajabu kunywa mkojo wako kama 'kipimo cha kuishi' katika dharura kama hiyo lakini watu wengi katika maeneo mbali mbali duniani wanaamini kwamba kunywa mkojo wako kuna manufaa kwa maisha 'ya kiafya'.
Lakini Je, kuamka asubuhi na mapema na kunywa mkojo wako mwenyewe kunatibu magonjwa? Je, kupaka mkojo kwenye mwili na uso huifanya ngozi kuwa na laini na yenye afya kama inavyoaminiwa? Madaktari wanasema nini kuhusu hili?
Kelly Oakley, mwalimu wa yoga mwenye umri wa miaka 33 anayeishi Uingereza, hivi majuzi alifichua kwamba kunywa mkojo wake mwenyewe kumemsaidia kukabiliana na matatizo ya muda mrefu. Alisema kuwa dawa hii imempa nafuu ya tezi dume na maumivu ya muda mrefu.
Kelly alilieleza hivi karibuni shirika la habari la Associated Press kwamba amekuwa akikunywa mkojo wake kwa miaka miwili iliyopita.
"Nilisikia kwamba kunywa mkojo kunaboresha mfumo wako wa kinga, husaidia kudumisha afya njema, na ni nzuri kwa ngozi yako," Kelly alisema. Kwa hivyo nilianza kujaribu jaribio langu la kunywa mkojo.
Si kunywa tu mkojo wake kila siku, lakini pia huupaka kwenye ngozi yake. Alisema kuwa dawa hii iliifanya ngozi yake kung'aa zaidi.
Watu wengi huita dawa hii 'tiba ya mkojo'. Dawa hii pia inajulikana kama 'Urophagia'.
Lakufurahisha ni kwamba, Kelly sio mtu pekee anayedai kufaidika kwa kunywa mkojo wake mwenyewe. Hivi karibuni kumekuwa na mifano mingi kama hiyo.
"Kunywa mkojo wangu mwenyewe kumenisaidia kupunguza nusu ya uzito wangu," Sampson, 46, wa Albert, Canada, aliliambia jarida la Sun.
Hapo awali alisema kuwa uzito wake ulipungua hadi kilo 120, jambo ambalo lilikuwa likimsumbua, lakini sasa tangu ameanza kunywa mkojo wake mwenyewe, uzito wake umerudi kawaida.
“Rafiki yangu alinitumia video akielezea tiba ya mkojo. Baada ya kutazama video hiyo, nilikwenda bafuni, nikajaza kikombe na mkojo wangu na kunywa. Ndani ya siku chache, nilianza kuona tofauti ndani yangu.”, alieleza.
Sasa wanakunywa mkojo kila siku na pia kutumia mkojo wao kusukutua vinywa vyao wakati wa kupiga mswaki asubuhi. Pia huweka matone yake machoni pao.
Mwanamke mwingine, Faith Canter mwenye umri wa miaka 39 kutoka Ureno, hivi karibuni alisema kwamba anakunywa mkojo wake ili kupunguza maumivu ya kuumwa na mbu.
Alisema, “Nilihisi ajabu kidogo mwanzoni, lakini taratibu nilizoea. Ninakunywa mkojo kila asubuhi. Sasa naumwa na mbu kidogo kuliko zamani. Na hata ikiumwa wakati mwingine, hakuna uvimbe, kuwasha wala maumivu.”
Kujua maoni mengi mazuri kuhusu 'tiba ya mkojo', ni kawaida kwamba maswali huibuka akilini kuhusu faida zake. .
Social Plugin