Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi- Dar es salaam.
Hospitali Kuu ya Jeshi la Polisi iliyopo wilaya ya Temeke Barabara ya Kilwa Mkoa wa Dar es salaam itanufanika na mafunzo ambayo yatatolewa kwa muda wa siku mbili na shirika la Quality Heathcare Solution and Consulting (QHSC) ambalo lina husika na kutoa mafunzo kwa watoa huduma za afya makazini ili kuwajengea uwezo madaktari kutoa huduma bora katika hospital hiyo.
Akiongea mara baada ya mafunzo kwa Madaktari na wauguzi kutoka hospitali kuu ya Jeshi la Polisi Dr. Harrieth Kokushubila Gabone ambaye ni Rais wa shirika hilo amesema wamefika katika hospitali hiyo kwa lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kuwasaidia wananchi wenye magonjwa ya moyo wanaofika kupata huduma katika hospital hiyo.
Ameongeza kuwa wamefika hapo na wataalam kutoka Marekani na watatoa mafunzo kwa muda wa siku mbili ambayo yamelenga kuwajengea mbinu ya namna ya kuokoa Maisha ya wananchi wenye changamoto ya magonjwa ya moyo.
Kwa upande wake Daktari mfawidhi wa hospital kuu ya Jeshi la Polisi Dk.Nyanda Lushina amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kufanikisha kuwaleta wataalam hao katika hosptali hiyo ambapo amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo Mkubwa kiutendaji.
Naye Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Emmanuel Shija ameshukuru shirika hilo kutoka marekani kwa kutoa elimu ambayo amebainisha kuwa elimu hiyo imekuja wakati muafaka kwao kwani wamekuwa wakipokea wagonjwa wenye changamoto ya magonjwa ya moyo.
Pia Konstable wa Polisi Daktari Davis Mwita kutoka kitengo cha Dharura Hospital kuu ya Jeshi la Polisi amebainisha kuwa mafunzo hayo yamewaongezea ujuzi na maarifa watakayo yatumia pindi wanapotoa huduma kwa askari Pamoja na wananchi wengine wanaofika katika hosptali hiyo kupata huduma.
Social Plugin