Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANANDOA SABA WAFANYA HARUSI YA PAMOJA KUPUNGUZA GHARAMA

Waumini wa Kanisa la Kianglikana la All Saints Kyamwee kaunti ya Machakos nchini Kenya wamefanyiwa harusi maalum iliyojumuisha wanandoa saba.

Kulingana na NTV, wanandoa hao walisema walikubaliana kufanya sherehe ya pamoja ili kugawana gharama kutokana na gharama ya juu ya maisha.

Kanisa lilijaa familia na marafiki na waumini wa kanisa waliofika kushuhudia wanandoa hao wakifunga pingu za maisha.

Wanandoa hao walielekea kanisani mmoja baada ya mwingine huku wakionyesha mitindo yao ya kupendeza ya kucheza. Wapenzi hao, mmoja baada ya mwingine, walivishana pete kabla yan kulishana keki kwa mikono yao.

 Mmoja wa wapambe hao, Alphonse Mwaziri mwenye umri wa miaka 74, alifichua kuwa alikuwa ameishi na mkewe mrembo kwa zaidi ya miaka 50. “Naishi na mke wangu kwa furaha naomba wale wa ukoo wangu waige mfano huo na wafunge ndoa zao kanisani,” alisema.
Joseph Mutungi, Padri aliyeungana na wanandoa hao saba, alikuwa na ushauri mzito kwa wengine. “Msiogope kuoa kanisani kwa sababu kuna tofauti kati ya harusi ya kanisani na harusi ya bustani,” alisema.

Wakenya wengi wameonekana kulikumbatia wazo hilo la harusi ya halaiki.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com