Na Dotto Kwilasa, Dodoma
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabir Shekimweri amesisitiza kuundwa kwa timu ya ufuatiliaji na tathmini ya zoezi la Anwani za Makazi ili kufanikisha azma ya Serikali ya kila Mtu kutambulika kirahisi mahali anapoishi.
Amesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa jamii kufikiwa na huduma za Kijamii kwa haraka ikiwa ni pamoja na huduma za biashara mtandao kuboreshwa.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Dodoma ameeleza hayo leo Sept 14,2023 Jijini Dodoma ,wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kuhusu Mfumo wa anwani za Makazi kwa Maafisa Tarafa,Maafisa Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Mitaa pamoja na Maafisa Watendaji wa Mitaa wa Jiji la Dodoma.
Aidha mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Habari,Mawasiliano naTeknolojia ya Habari Kwa lengo la kuboresha huduma za jamii na kuhuisha maisha kidigitali.
Kwa Upande wake Mratibu wa anwani za Makazi Kitaifa,Panton Mbugi ameeleza kuwa Mafunzo ni muhimu kwa kuwa yatalifanya Jiji la Dodoma kuwa la mfano katika kutekeleza zoezi hilo.
Nao washiriki wa mafunzo hayo,Wameishukuru Wizara ya Habari kwa mafunzo hayo na kuahidi kutekeleza kwa Vitendo.
Joshua Jembe ameeleza kuwa mafunzo ya anwani za makazi ni muhimu kwa Kila mtanzanzania Ili kurahisisha huduma za kijamii kwenda kidigitali na kutoka wakati.