SJMT NA SMZ YAWAPA WANAWAKE KIPAUMBELE KWENYE KILIMO CHA MWANI


Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapindizi Zanzibar (SMZ) zimekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inawapa nguvu Wanawake katika kuimarisha Kilimo Cha zao la Mwani.

Hayo yamesemwa leo Sept 27,2023 jijini Dar es salaam katika viunga vya ofisi ya Mtandao wa jinsia TGNP na Mwezeshaji wa Semina ya jinsia na Maendeleo Bw.Kennedy Anjelita ambapo Semina hizo zimekuwa zikitolewa kila Jumatano.

"Serikali ya Jamuhuri imetoa boti kwa ajili ya Kilimo cha zao la Mwani huko Kilwa ambapo Rais Samia katika ziara yake hivi karibuni aliwapa wanawake kipaumbele kwenye Kilimo na ufugaji"Amesema

Aidha Bw.Kennedy amelalamikia mfumo dume inayoendelea katika baadhi ya familia ambao una mkandamiza mwanamke katika kilimo na ufugaji.

"Tanzania na bara la Afrika mwanamke anashiriki katika Kilimo na upishi lakini kwenye kulimo wanawake hawanufaiki kabisa ninaamini kwa Mama Samia atafanyanya mabadiriko kwasababu wanawake watamiliki uchumi wao wenyewe na wanaume itabidi wakubaliane na hali"Amesema

Pamoja na hayo amesema wanawake wakazidishe juhudi katika Kilimo na kumiliki taasisi ambazo zinajihusisha na masuala ya Kilimo.

"Kilimo kimekuwa biashara Tanzania imepokea ugeni wa nchi zaidi ya 54 watu Hawa tukiwa na uzalishaji mzuri soko lipo na ikiwezekana wanawake waachane na masuala ya kumiliki vikundi wajikite kumiliki kampuni za Kilimo ili kukuza thamani"Amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم