TFS YAWAHAMASISHA WATANZANIA KUTEMBELEA VIVUTIO

 


 Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Tanzania Forest Services (TFS),wamewaalika watanzania wote kutembelea misitu ya TFS kwani kuna vivutio vizuri na mazingira yake ni yakuvutia.

Akizungumza katika kilele cha hitimisho ya wiki ya Kongamano la pili la kitaifa la ufuatiliaji, Tathmini na mafunzo Bi.Anna Lawuo ambaye pia ni Afisa mtalii amesema kuwa TFS wanavyo vivutio vingine mbali na tofauti vile ambavyo wamevizoea ambavyo ni vivutio vya utalii Ikolojia vinavyopatikana ndani Misitu ya hifadhi hiyo ikiwemo ziwa lenye ramani ya Afrika.

Vilevile Bi. Anna amesema kuwa ndani ya misitu hiyo kuna fursa za uwekezaji na upatikanaji wa bidha za nyuki ambapo kutokana na  mizinga hiyo ya nyuki inaweza kuwapatia faida kwa sababu mizinga hiyo inatoa bidhaa mbali mbali zinazotokana na nyuki ikiwemo asali na nta ambayo wameitumia kutengenezea bidhaa mbalimbali zinazotokanazo na nta hiyo ya nyuki.

Pamoja na hayo alisema kuwa kwa wale watanzania wanaofanya mazoezi barabarani wana uwezo wa kwenda kufanyia mazoezi katika misitu hiyo kwa sababu hali ya hewa iliyopo maeneo hayo ni nzuri na ni safi pia kwa afya ya mtu yoyote "Tunawaomba wale wanaofanya mazoezi mijini wanaofanya kwenye barabara sehemu ambazo kuna mwingiliano wa watu wengi na magari si salama sana kwa afya lakini wakija maeneo ya  msituni watakutana na hewa safi na utakuwa umepumzika kwa kuvuta hewa safi ambayo haitaathiri mwili wako"alisema.

Hata hivyo alimazia kwa kusema kuwa watalii na watanzania wote wanakaribishwa katika misitu hiyo kwa sababu kuna maeneo ya kempu na mandhari ya kuvutia huku kiingilio chake kikiwa rahisi kwa mgeni na mtanzania yoyote atakayetamani kutembelea vivutio hivyo.

Naye mhifadhi mwandamizi kutoka TFS,Kelvin Fella amesema kuwa ndani ya utalii ekolojia kuna hifadhi za malikale kuna vivutio vingi vyakuanzia enzi za ukoloni mpaka tulipopata Uhuru kukiwa na vituo tofauti kama mji mkongwe unaopatikana Bagamoyo ikiwa ndiyo mji mkuu wa kwanza vikiambatana na magofu ya Kaole ambayo ni vivutio vikubwa kwa watalii.

Alisema kuwa kutembelea vivutio hivyo ni gharama nafuu "katika hifadhi za Bagamoyo na Kaole ni kiingilio nafuu kwa Mtanzania ni Shilingi elfu mbili tu huku mgeni ni elfu ishirini ya Kitanzania na kwa mgeni ambaye ni wa moja kwa moja atalipa elfu kumi tu unaweza kulipa na kupata historia katika vivutio hivyo "alisema.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post