Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi akizungumza wakati akifungua Warsha ya Mafunzo ya ufuatiliaji na uwajibikaji kwa Mashirika na Asas leo Septemba 4,2023 katika Ofisi za TGNP Jijini Dar es Salam
*****
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
MASHIRIKA na Asasi za Kiraia nchini kuungana pamoja katika kuhakikisha wanawawezesha wanawake na wasichana kusambaratusha mifumo dhalimu na kuunda mustakabli ambapo usawa wa kijinsia si matarajio tu bali ni ukweli unaoishi kwa wote.
Wito huo umetolewa leo Septemba 4,2023 Jijini Dar es Salaam,na Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi wakati akifungua Warsha ya Mafunzo ya ufuatiliaji na uwajibikaji kwa Mashirika na Asasi.
Alisema kuna umuhimu wa kuingana pamoja katika dhamira ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake.
"Ebu tukibaliane na uwezo wa kuleta mabadiliko chanya kwa kuyapa mashirika na washirika wetu ujuzi na zana zinazohitajika ili kuleta mabadiliko ya kudumu katika jumuiya yetu". Alisema
Aidha Bi.Liundi alisema mafunzo hayo yanalenga kuyapa mashirika ya haki za wanawake zana na maarifa muhimu ya kufanya ufuatiliaji na tathmini ambayo inaakisi mabadiliko na matokeo chanya katika jamii kwa jicho la kijinsia au kifeminia .
Alisema Mafunzo hayo yatawezesha mashirika kutathmini ufanisi wa programu zao, kutambua maeneo ya kuboresha na kuonyesha mafanikio yao kwa wengine.
Kwa upande wake Mwezeshaji katika warsha hiyo, Bi. Mary Msemwa alisema kuwa wanategemea washiriki watakuwa na uelewa mkubwa wa namna ya kufanya ufuatiliaji na utathmini kwa mlengo wa kifeminia katika mashirika yao.
Nao washiriki wa semina hiyo wamesema watajifunza mambo mengi ambayo wlaikuwa hawayafahamu kuhusu masuala ya usawa na haki za wanawake na pia watayatumia mafunzo hayo na kuongeza ufanisi kwenye taasisi zao.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi akifungua Warsha ya Mafunzo ya ufuatiliaji na uwajibikaji kwa Mashirika na Asas leo Septemba 4,2023 katika Ofisi za TGNP Jijini Dar es Salam
Washiriki wa warsha ya Mafunzo ya ufuatiliaji na uwajibikaji kwa Mashiriki na Asasi