Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TIMU YA UVCCM MASEKELO YAONDOLEWA KIBABE NA TIMU YA UVCCM NGOKOLO KATIKA MASHINDANO YA DKT. SAMIA CUP SHINYANGA

Mratibu wa Mashindano ya Dkt.Samia Cup Jackline Isaro akiendelea kufuatilia mwenendo wa mashindano katika uwanja wa Shy Com. 

Namwandishi wetu Malunde Blog Shinyanga 

Wakati Mashindano ya Dkt. Samia Cup yakiendelea kutimua vumbi katika viunga mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kumtafuta bingwa atakayeibuka na zawadi mbalimbali katika mashindano hayo,Timu ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCC) kata ya Masekelo imekubali kutolewa kibabe na Timu ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kata ya Ngokolo katika Mtanange uliopigwa katika uwanja wa Chuo cha walimu Shinyanga (Shy Com) ikiwa ni hatua ya 16 bora ya kutafuta timu zitakazo shiriki hatua ya Robo fainali.

Katika mchezo huo Timu ya UVCCM Masekelo imeshindwa kutamba mbele ya Timu ya UVCCM Ngokolo baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika bila kufungana huku timu hiyo ikishindwa kufurukuta katika upigwaji wa mikwaju ya penalti ambapo timu ya UVCCM Ngokolo imefunga penalti tano kwa nne dhidi ya timu ya UVCCM Masekelo na kuifanya timu ya Masekelo kuaga katika mashandano hayo huku UVCCM Ngokolo ikipata tiketi ya kwenda kushiriki katika hatua ya robo fainali.

Pia katika mchezo mwingine Timu ya Ngokolo Sekondari imekubali kuaga mashindano hayo baada ya kupokea kichapo cha magoli mawili kwa sifuri kutoka kwa Timu pinzani ya Wapigadebe kutoka kata ya Ndembezi.

Mratibu wa Mashindano ya Dkt.Samia Cup Jackline Isaro akiendelea kufatilia mwenendo wa mashindano katika uwanja wa Shy Com. 
Wamuzi wa mchezo wakijiandaa kwa ajili ya mpambano katika uwanja wa Shy com
Timu ya UVCCM Ngokolo baada ya kupata ushindi.
Vijana wa hamasa kutoka Masekelo Wakiendelea na hamasa wakati wa mchezo.
Vijana wakipata burudani katika uwanja wa Shy Com.

Vijana wahamasa kutoka Masekelo Wakiendelea na hamasa wakati wa mchezo.

Vijana wahamasa kutoka Ngokolo Wakiendelea na hamasa wakati wa mchezo.
Wadau wamichezo wakiendelea kutazama burudani.


Wadau wamichezo wakiendelea kutazama burudani.

Timu ya Ngokolo Sekondari ikipambana na Timu pinzani ya Wapigadebe kutoka kata ya Ndembezi katika uwanja wa kitangili.
Timu ya Wapigadebe kutoka kata ya Ndembezi ikipambana na Timu ya Ngokolo Sekondari kutoka katika kata ya Ngokolo
Timu ya Ngokolo Sekondari ikiwaza baada ya kutolewa katika mashindano na timu ya Wapigadebe fc kutoka katika kata ya Ndembezi 
Timu ya Wapigadebe kutoka kata ya Ndembezi wakipanga mbbinu za kuiondoa Timu ya Ngokolo Sekondari katika Mashindano 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com