WANAHARAKATI wamepewa ujuzi wa kukabiliana na changamoto ya afya ya akili wakiwa katika mazingira ya kazi au nyumbani ili kuhakikisha kupungua kwa matatizo hayo kwenye jamii ambapo inaonekana tatizo hilo limekithiri.
Akizungumza leo Septemba 13,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwezeshaji wa Semina hiyo Bi.Sylivia Sosthenes amesema kupitia semina hiyo itasaidia kuangalia wanaharakati na Afya zao za akili na yale wanayo kumbana nayo katika harakati, kuanzia familia zao,wanakutana na kesi ngapi na lipi suluhisho la Afya zao za Akili.
"Matokeo ya Semina hii ni kuepuka matukio ambayo ni ya kikatili yasipelekee Changamoto ya Afya ya akili ".
Aidha Bi Sylivia amesema sababu zinazo pelekea matatizo ya Afya ya akili,ni pamoja na ukatili wa kijinsia, Changamoto za kiuchumi,maswala ya malezi, mahusiano kazini au nyumbani.
Pamoja na hayo amesema dalili za Changamoto ya Afya ya akili Ni pamoja na mtu kujitenga,mtu kutokujijali au kuleta viashiria vya kujitoa uhai au kumtoa mtu uhai.
"Mtu mwenye tatizo la Afya ya akili kwa mtu ambaye si mtaalamu anatakiwa amuoneshe sehemu ya kwenda au kumpatia ushauri wa awali,na kwa mtu ambaye Ni mtaalamu anatakiwa kumshauri na kumfanyia rufaa kwa wataalamu wengine,maana Changamoto hii ina athiri wakati mwingine Hadi mwili." amesema
Social Plugin