Na Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kushuka chini kwa wananchi ili kusimamia fedha za miradi yote iliyotolewa na Serikali.
Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Septemba 4, 2023 wakati akiwahutubia watumishi wa TAMISEMI baada ya kukabidhiwa Ofisi na Waziri wa zamani wa ofisi hiyo Mhe. Angellah Kairuki mtumba jijini Dodoma.
Amesema serikalai imetopa fdedha nyingi katika miradi mbalimbali kwa wananchi hivyo viongozi walio katika mikoa na Halmashauri za wilaya wanawajibu wa kuhakikisha kuwa wanasimamia ili kutimiza malengo ya Serikali.
Ndugu zangu naomba nisisitize kuwa dhamira ya serikali kwa sasa ni kuona kuwa kila fedha inayotolewa inafanya kazi kwa faida ya wananchi.
Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kusimamia wizara hiyo na kutenga fedha nyingi za miradi ya maendeleo kwa wananchi ampo pia amemhakikishia kuwa atakwenda kusimamia kikamilifu kwa kushirikiana na menejimenti ya Wizara hiyo.
Aidha amesema katika kipindi chake wizara itazingatia utendaji wa haki na wajibu na kwamba watumishi wazembe na wasio waadilifu watachukuliwa hatua.
Akizungumzia kuhusu ufanyaji wa kazi Mhe. Mchengerwa amesema watumishi wanatakiwa kutambua kuwa wameaminiwa na serikali hiyo wanatakiwa kuwa wazalendo wakati wote wanapofanya kazi ili kuleta maendeleo.
Pia amesisitiza kwamba katika kipindi chake hataongeza kipindi cha utekelezaji wa miradi kwa wakurugenzi wote na badala yake amewataka wakamilishe miradi hiyo katika kipindi ambacho waliahidi kuimaliza.
Waziri Mchengerwa anakuwa ni waziri aliyeshika nafasi ya uwaziri katika wizara nne tofauti katika kipindi cha miaka miwili, wizara hizo ni pamoja na UTUMISHI, Utamaduni Sanaa na Michezo, Maliasili na Utalii na sasa TAMISEMI.
Social Plugin