KLABU ya Yanga SC imefanikiwa kutinga hatua ya makundi michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuichapa Al Merreik ya Sudan bao 1-0 mchezo ambao umepigwa kwenye dimba la Chamazi.
Kwa mara ya mwisho Yanga SC kufuzu hatua ya makundfi ilikuwa mwaka 1998 takribani miaka 25.
Akichukua nafasi ya Kennedy Musonda,Mshambuliaji Clement Mzize aliwanyanyua wananchi waliofurika uwanja wa Chamazi akifunga bao dakika ya 66 kwa kichwa akimalizia krosi ya Joyce Lomalisa.
Yanga SC wametinga hatua ya makundi kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Rwanda,Yanga walishinda mabao 2-0.
Sasa rasmi Yanga SC inaungana Pyramids FC,Al Ahly zote za Misri,Jwaneng Galaxy ya Botswana,TP Mazembe ya DR Congo,Ptro Atletico ya Angola,Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini,Medeama SC ya Ghana.
Michuano hiyo itaendelea kesho katika uwanja wa Azam Complex Chamazi wekundu wa Msimbazi Simba SC watawakaribisha Power Dynamos kutoka Zambia huku Simba wakihitaji ushindo wowote au sare yoyote wakiwa na faida ya mabao 2 ya ugenini mara ya mechi ya kwanza kufungana mabao 2-2.
Social Plugin