Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BYABATO AAPISHWA KUWA MBUNGE WA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


Jana tarehe 03/ 10/2023 Wakili Stephen Byabato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alikula kiapo cha kuwa Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Pia Wakili Stephen Byabato(Mb) jana alishiriki Mkutano wa Dharura wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliofanyika kwa njia ya Mtandao Jijini Dar es salaam kujadili bajeti ya Jumuiya kwa Mwaka 2023/2024, Mkutano huwo ulihudhuriwa na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka nchi na Wanachama wa Jumuiya hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com