Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMBO SUPER LEAGUE KUANZA KUTIMUA VUMBI KESHO...TIMU MPYA YANUKIA

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Michuano ya Ligi ya Jambo ‘Jambo Super League’ inayohusisha Timu 10 za Wafanyakazi  kutoka Idara mbalimbali katika Kampuni ya Jambo Group (Jambo Group of Companies) itaanza kutimua vumbi kesho Jumapili Oktoba 29,2023 katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom) Mjini Shinyanga.

Akizungumza na Vyombo vya Habari leo Jumamosi Oktoba 28,2023, Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa Kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi amesema Mshindi wa kwanza katika Ligi hiyo ataondoka na Kitita cha Shilingi Milioni  2, Kombe na Medali huku mshindi wa pili akiondoka na zawadi ya shilingi Milioni 1.8 na medali wakati mshindi wa tatu akipata shilingi Milioni 1.

“Jambo Super League itaanza Jumapili Oktoba 29,2023 saa nane mchana katika Uwanja wa Shycom na watakaotufungulia kesho ni Timu ya Jambo Store na Jambo Transport, mechi ya pili itakayoanza saa 10 jioni  ni kati ya Jambo Biscuit na  Jambo Plastic ambayo itafanyika hapo hapo Shycom”,amesema Kabudi.

Ameeleza Mechi zote zitachezwa kila Jumapili  kwa muda wa Wiki 7 kuanzia Oktoba 29,2023 hadi Desemba 17,2023 ikihusisha timu 10 mpira wa miguu za Wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Group kutoka Idara mbalimbali ambazo ni Ice Cream, CSD, Biscuit, Store, Jambo Media & Administration, Plastic, Zoo, Garage, Bakery na Printing.

“Viwanda vyetu ni vingi, lengo la ligi hii ni kuwaleta pamoja wafanyakazi wa Kampuni  ya Jambo Group ni kufahamiana,tujuane, tufanye mazoezi pamoja kwa sababu nusu ya siku tunaitumia hapa kama ndugu. Kila mwaka tumekuwa tukiwaleta wafanyakazi pamoja kwa namna tofauti. Lakini mwaka huu tumeona tuwalete pamoja kivingine kimichezo ili humo wapate pia afya, tugundue vipaji vingine pengine siku moja tutakuwa na timu ya Mpira ya Jambo FC/Jamukaya itakayoshiriki ligi ngazi ya wilaya, mkoa na Ligi kuu”,ameongeza Kabudi.

“Nitumie fursa hii kuwaomba wadau wote wajitokeze kuunga mkono juhudi za Wafanyakazi na Kampuni ya Jambo Group kuwaleta wafanyakazi pamoja, kufurahi pamoja na kufanya mazoezi pamoja”,amesema.

Mbali na kutambulisha Kamati yenye wajumbe wasiopungua watano ambapo mmoja wao atatoka katika Chama Cha Mpira wa Miguu  Mkoa wa Shinyanga, Kamati ya Maamuzi, Huduma ya Kwanza, mwingine kutoka kitengo cha Michezo Jambo Media, pia Kabudi amekabidhi Jezi kwa timu zinazoshiriki Jambo Super League.
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa Kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akizungumza na Vyombo vya Habari leo Jumamosi Oktoba 28,2023 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa Kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akizungumza na Vyombo vya Habari leo Jumamosi Oktoba 28,2023
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa Kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akionesha moja ya jezi zitakazotumika katika Jambo Super League

Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa Kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akikabidhi Jezi kwa timu zinatakazoshiriki Jambo Super League

Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa Kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akikabidhi Jezi kwa timu zinatakazoshiriki Jambo Super League.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com