Naibu Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Ridhiwani Kikwete akihutubia katika mahagali ya pili ya kidato Cha nne katika Sekondari ya Pera, Halmashauri ya Chalinze
NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mh. Ridhiwani Kikwete ameahidi ujenzi wa mabweni mawili katika shule ya Sekondari ya Pera katika halmashauri ya Chalinze mkoa wa Pwani.
Mh. Ridhiwani alitoa ahadi hiyo alipokuwa akihutubia umati wa wazazi ,walimu na viongozi mbalimbali katika mahafali ya pili ya kidato Cha nne shuleni hapo leo.
Mh. Ridhiwani ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hiyo alisema kuwa pamoja na shule kuwa na chamgamoto ya bweni moja ,yeye ameona umuhimu wa kuwajengea mabweni mawili ili kusaidia wanafunzi hao kutopata shida ya kutembea umbali mrefu kutoka nyumbani hadi shuleni.
Mh. Kikwete ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Chalinze pia ameahidi kumsomesha mwanafunzi mwenye ulemavu aliyejiunga na Elimu ya chuo mkoani Arusha hadi atakapohitimu mafunzo yake.
Kabla ya mgeni rasmi kuzungumza, Diwani wa kata ya Pera Mh. Jackson Mkango na Mwenyekiti wa CCM wa kata ya hiyo, Bw. Kaisi Chombo wamewatakia wanafunzi hao wa kidato Cha nne mtihani mwema na kusema iwapo shule itapatiwa mabweni, itasaidia sana kuleta ufanisi katika upatikanaji wa taaluma shuleni hapo.
Naye Mkuu wa shule hiyo Bw. Alex Kamaga katika risala yake alieleza kuwa shule ina changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa bweni moja kwaajili ya wanafunzi wa kike, nyumba za walimu pamoja na vyoo vya wanafunzi.
Jumla ya wanafunzi 158 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu kidato Cha nne katika shule hiyo.
Naibu Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Ridhiwani Kikwete akihutubia katika mahagali ya pili ya kidato Cha nne katika Sekondari ya Pera, Halmashauri ya Chalinze
Social Plugin