Afisa elimu na mawasiliano TRA Mkoa wa Kagera Bw. Rwekaza Rwegoshora akitoa elimu kwa waandishi wa habari
Na Mbuke Shilagi - Kagera.
Mamalaka ya Mapatao Tanzania (TRA) Mkoa wa Kagera imetoa elimu kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Kagera kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi.
Akizungumza leo katika ukumbi wa E.L.C.T uliipo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Afisa Elimu na Mawasiliano TRA Mkoa wa Kagera , Rwekaza Rwegoshora amesema kuwa wajibu wa mlipa kodi na mfanyabiashara yoyote ni kutunza kumbukumbu ya mauzo ambayo itamsaidia katika makadirio na itamfanya alipe kodi sahihi.
Amesema kuwa kulingana na sheria, mfanyabiashara ambaye anaingiza milioni 11 na zaidi kwa mwaka anatakiwa kuwa na EFD mashine kwa lengo la kulipa kodi ambayo ni sahihi na itakayofanya kujua maendeleo ya biashara yake.
Aidha Rwegoshora amewataka wananchi wote kudai risiti mara baada ya kununua bidhaa na wafanyabiashara kutoa risiti mara baada ya kuuza bidhaa na anayebainika hajafanya hivyo atalipa faini na akibainika ameuza na hajatoa risiti atalipa faini ya milioni moja na nusu au asilimia 20 ya bidhaa au huduma na kwa mnunuzi akibainika hajadai lisiti atalipa faini ya 20,000 au asilimia 20 ya bidhaa.
"Hizi adhabu siyo kuwakomoa wananchi au wafanya biashara nikwaajili ya kuwalinda ili sasa waanze kutekeleza kudai au kutoa lisiti",amesema Bw. Rwegoshora
Afisa Elimu na Mawasiliano TRA makao makuu Bw Isihaka Sharifu akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Afisa Elimu na Mawasiliano TRA makao makuu Bw Isihaka Sharifu akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Waandishi wa habari wa mkoa wa Kagera waliohudhuria mafunzo ya TRA
Social Plugin