(𝐈𝐦𝐞𝐚𝐧𝐝𝐢𝐤𝐰𝐚 𝐍𝐚 𝐌𝐰𝐚𝐧𝐝𝐢𝐬𝐡𝐢 𝐖𝐞𝐭𝐮)
MKUU wa Wilaya ya Songwe, Solomon Itunda amewataka vijana kuacha kubabaika na kupagawa na wanawake wenye makalio makubwa (mizigo) hali inayosababisha kuhonga mpaka mitaji yao ambapo amewakumbusha kuwa baadhi ya mizigo ina gharama zake ikiwemo kufilisi vijana mitaji na hata kupata magonjwa.
Itunda amesema hayo wakati wa kongamano la kujadili namna ya kuzuia ajali wilayani humo lililowahusisha zaidi ya vijana 1,000 ambao ni madereva wa bodaboda, bajaji, guta, noah na taksi lililofanyika katika Mji wa Mkwajuni ambapo amesema wakati mwingine madereva husababisha ajali kutokana na kuwaangalia wanawake hao wakati wao wakiwa wanaendesha.
CHANZO - NIPASHE