Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe leo Oktoba 29,2023 amemtaka mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa mradi wa (EASTRIP) kuja na mpango kabambe wa kufidia muda uliopotea.
Prof.Mdoe amesema hayo alipotembelea Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) -Kampasi ya Mwanza kukagua maendeleo ya mradi wa kituo Cha Kikanda cha Umahiri wa Bidhaa za Ngozi (EASTRIP) na kukuta mradi ukiwa katika hali isiyoridhisha kuzingatia makubaliano ya mkataba na muda uliobaki kukamilisha mradi huo.
Prof. James ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kwamba ,alitaka kuona pale mradi ulipofikia tangu afike, Januari,2023, ili ajiridhishe na maendeleo ya mradi,ajue changamoto ni zipi kwa upande wa wizara ili kazi ikamilike kwa wakati.
Aidha, Prof. Mdoe amesisitiza kazi ya ujenzi wa kituo hicho isimamiwe kwa ukaribu na mara kwa mara ili mkandarasi amalize kwa haraka lakini pia kazi ifanyike Kwa ubora.
"Serikali inataka kuona thamani ya pesa inayotumika ikionekana katika mradi huu,kazi ifanyike kwa haraka lakini kwa umakini mkubwa na siyo kwenda na kasi tu"
,amesema prof. James.
Hata hivyo Prof. Mdoe mbali na kutaka uwepo mpango kabambe wa kufidia muda uliopotea pia amemtaka Mratibu wa mradi huo Dkt, Albert Mmari kuhakikisha anasimamia kazi zote ambazo hazijakamilika zifanyike mapema sana ili kuiwezesha taasisi ya DIT-Mwanza kupokea wanafunzi wengi zaidi katika mwaka wa masomo wa 2024/2025.
Mradi huo wa kituo cha kikanda cha Umahiri wa Bidhaa za Ngozi (EASTRIP) wenye thamani ya dola za Kimarekani
USD 16.25 milioni unatakiwa kukamilika mwezi Desemba, 2024.
Social Plugin