Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

OFISI YA WAZIRI MKUU YAENDELEA KUTOA TAHADHARI MVUA YA EL NINO


Na Jaliwason Jasson, BABATI

OFISI ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Idara ya Menejimenti ya Maafa imesema inatumia Programu zinazopendwa na makundi ya watoto na akina mama ili kuwapatia elimu juu ya maafa na tahadhari ya kuepuka mvua za El Nino zinazotarajiwa kunyesha.

Hayo yamebainishwa  leo na Mkurugenzi msaidizi ofisi ya waziri mkuu sera, Bunge na uratibu anayesimamia kituo cha operesheni na mawasiliano ya dharura Prudence Constantine wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya kimataifa ya kupunguza madhara ya Maafa ambayo hufanyika kila Oktoba 13.

 Amesema kupitia tamthiliya, maigizo na matangazo ndivyo wanavitumia kutoa elimu ya Maafa.

Aidha amesema wakitaka kuwapatia elimu watoto wanawafuata shuleni huku akisema wazee ambao nao ni kundi muhimu wanawafuata majumbani kwao.


Mkurugenzi huyo amesema elimu hiyo wanaitoa bure kwa wananchi ili kuwaepusha na Maafa ya mvua za El Nino.

Amesema wananchi wanaokataa kutoka maeneo hatarishi ya mabondeni na kutaka fidia wakumbuke kuwa fidia haiwezi kulingana na uhai wao.


Mtaalamu huyo wa Maafa amesema elimu hiyo wanayoitoa inaendana na maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupunguza madhara ya Maafa inayoadhimishwa kila Oktoba 13 kila mwaka.


Ameitaja mikoa inayotarajiwa kuathiriwa na mvua za El Nino kuwa ni Kagera, Geita,Mwanza, Shinyanga, Simiyu,Kigoma,Dar es salaam, Tanga,Pwani, Morogoro,Unguja Kusaini,Manyara, Unguja Kaskazini  na Pemba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com