Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amewataka wamiliki wa shule zisizo za serikali kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa mujibu wa sheria ili kuleta tija kazini.
Akizungumza Oktoba 10, 2023 jijini Dodoma kwenye kikao na wamiliki hao kilichoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Katambi amesema kumekuwa na malalamiko kuhusu suala la michango ya NSSF na kwamba kupitia kikao hicho serikali itawasikiliza na kutafutia ufumbuzi suala hilo.
Aidha, amewataka kutafutia ufumbuzi migogoro ya kikazi kwenye maeneo yao kwa kuzingatia Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini ili shule zisiyumbe.
Social Plugin