Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI VIJIJINI 'RUJAT' WAFANYIKA DODOMA, MEENA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Neville Meena akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT) kimefanya Mkutano Mkuu wa Mwaka pamoja na uchaguzi wa viongozi ambapo Neville Meena aliyekuwa Katibu wa muda amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa RUJAT, Prosper Kwigize aliyekuwa Mwenyekiti wa muda akichaguliwa kuwa Katibu Mkuu, Editha Majura Mweka Hazina na Zania Miraji Kweka akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti. 

Katika Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023, pia wajumbe sita kulingana na Kanda wamechaguliwa ambao ni Anne Rhobi (Pwani), Meshack Ngumba (Magharibi), Hamida Ramadhani(Kati), Musa Juma (Kaskazini), Neema Emmanuel (Kanda ya Ziwa) na Felix Mwakyembe (Kusini).

 Mkutano huo umeenda sambamba na maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki ya kupata taarifa ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28, ambapo RUJAT ilikuwa na kauli mbiu ya changamoto za mawasiliano ya kidijitali vijijini ni kikwazo cha upagikanaji na usambazaji wa habari.

Maadhimisho hayo yamefadhiliwa na Mamlaka ya Uhifadhi Tanzania TANAPA, kampuni ya madini ya serikali STAMICO, Wakala wa Nishati Vijijini REA na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mkoa wa Tabora TUWASA.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Neville Meena amesema kazi kubwa sasa ya chama hicho ni kupata wanachama wengi zaidi ili kujenga RUJAT yenye nguvu. 
 
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa RUJAT , Proper Kwigize ambaye ni Mwenyekiti Muasisi wa RUJAT, amesema lengo la Chama hicho ni kuondoa utofauti wa vijijini na mijini kwani katika maeneo mengi ya vijijini hawapati taarifa habari mfano pale majanga yanatokea vijijini wananchi hawapati taarifa.

“RUJAT ni chama cha kipekee sana, hivi sasa kina wanachama 38. Tunataka kuandika habari za kusisimua maendeleo vijijini,tunataka kuondoa mitazamo ya kwamba hakuna haja ya kuandika habari za vijijini. Vyombo vya habari vinafanya vizuri kutokana na kwamba kuna waandishi wa habari vijijini. Uandishi wa habari vijijini ni muhimu sana, hakuna Tv, Redio, Gazeti linatukimbia sisi waandishi wa habari za vijijini”,amesema Kwigize.

Amesema RUJAT imepanga kufungua tovuti ambayo itakuwa inachapisha habari mbalimbali za vijijini ambayo itakuwa inatumiwa na waandishi wa habari kusambaza habari wanazoandika.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Neville Meena akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Neville Meena akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Neville Meena akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Neville Meena akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT),Prosper Kwigize akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT) ,Prosper Kwigizeakizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT),Prosper Kwigize akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT), Prosper Kwigize akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023

Mweka Hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT) Editha Majura akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023

Mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (Rural Journalists Association of Tanzania (RUJAT) , Felix Mwakyembe akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa RUJAT uliofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Jumapili Oktoba 1,2023
Afisa kutoka Benki ya NMB, Jastine Bandoma  akitoa elimu kuhusu Bima zinazotolewa na Benki ya NMB

 Afisa kutoka Benki ya TCB,Azory Mpungo akitoa elimu kuhusu Bima zinazotolewa na Benki ya TCB

Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wanachama wa RUJAT wakipiga picha ya kumbukumbu

Viongozi wapya wa RUJAT wakipiga picha ya kumbukumbu
Viongozi wakuu wa RUJAT wakipiga picha ya kumbukumbu
Viongozi wakuu wa RUJAT wakipiga picha ya kumbukumbu na mdau kutoka Benki ya TCB
Viongozi na wanachama wa RUJAT wakipiga picha ya kumbukumbu na mdau kutoka Benki ya NMB.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com