Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WASHINDI WA CHEMSHA BONGO NA SALOME WALAMBA ZAWADI TENA, WAJASIRIAMALI, STAND UNITED WAPEWA MAOKOTO

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Salome Makamba.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba amekabidhi zawadi kwa Washindi wa awamu ya tatu ya Programu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba huku akiweka wazi kuwa Programu hiyo itaendelea kuwepo kutokana na kupokelewa vizuri na wananchi.

Hafla ya kukabidhi zawadi imefanyika leo Jumamosi Oktoba 21,2023 katika Viwanja vya Redio Faraja na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

Katika Programu hiyo ya Chemsha Bongo na Salome Makamba inayoendeshwa na Kituo cha Matangazo Redio Faraja Fm Stereo kwa kushirikiana na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba washindi wamekabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo Majiko ya Gesi, Jezi na Mipira, madaftari, taulo za kike pamoja fedha kwa ajili ya kuviongezea mtaji wa bila riba wala marejesho vikundi mbalimbali vikiwemo vya wanawake, vijana, wazee na wenye ulemavu.

Pia Mhe. Makamba amekabidhi mchango wa Shilingi Milioni moja kwa Timu ya Stand United inayoshiriki Ligi ya NBC Championship ili kuishika mkono kampuni ya Jambo Food Products, mdhamini mkuu, ikiwa ni sehemu ya hamasa ya kuiongezea nguvu ya kiuchumi ifanye vizuri kwenye michezo yake na kuendelea kuuwakilisha mkoa wa Shinyanga.

Akikabidhi zawadi kwa washindi, Mhe. Makamba amewapongeza wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Chemsha Bongo na Salombe inayoendeshwa kupitia vya Redio Faraja.

Makamba amewakaribisha wadau mbalimbali kuunga mkono Programu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba huku akisisitiza kuwa  Programu hiyo itaendelea kuwepo, baada ya kumaliza awamu hiyo ya kwanza inayoishia mwanzoni mwa mwezi Novemba 2023.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Salome Makamba.

“Nipende kuipongeza  Redio Faraja kwa kutumia utaalamu wao vizuri na kuendesha Programu hii kwa weledi, uaminifu na uadilifu mkubwa, pasipo upendeleo. Tangu tumeanza sijasikia malalamiko yoyote zaidi ya kupokea simu nyingi za pongezi kutoka kwenye makundi mbalimbali kwenye jamii. 

Redio Faraja mmeonesha weledi wa hali ya juu, endeleeni hivyo, maana natambua kuwa chombo cha habari kufanya kazi na sisi wanasiasa bila kukwaza upande mwingine ni kazi ngumu inayohitaji umakini mkubwa”,ameongeza Mhe. Makamba.

Meneja vipindi wa Redio Faraja na Mratibu wa Chemsha Bongo na Salome Makamba, Simeo Makoba ameeleza kuwa Redio Faraja kupitia Falsafa yake ya ‘Tunajenga Jamii’, imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na kwa karibu na wadau wengine ikiwemo serikali kuhakikisha jamii nzima inaishi kwa usalama, furaha, umoja, upendo, amani na mshikamano.
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi mshindi wa  Chemsha Bongo na Salome Makamba

Amesema Redio Faraja inatekeleza wajibu huo kwa weledi mkubwa bila upendeleo kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari, hatua ambayo imeifanya kuwa ni chombo cha habari kinachoaminika kwa watu.

Makoba amebainisha kuwa, kutokana na msimamo wa Redio Faraja wa kuangalia zaidi maslahi mapana ya jamii, ilipata msukumo wa kushirikiana na Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Salome Makamba, baada ya kujiridhisha kuwa ana nia njema ambayo inaendana na falsafa yake ya Tunajenga Jamii’.

“Kupitia Chemsha Bongo na Salome Makamba, licha ya kuwawezesha wasikilizaji wake na wananchi kushinda zawadi mbalimbali, pia ni njia mojawapo ya kuibua vipaji kupitia michezo na kuipa jamii msukumo wa kutafuta na kufuatilia taarifa mbalimbali zinazohusu maendeleo pamoja na kuvijengea uwezo wa kiuchumi vikundi vya wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu”,ameeleza Makoba.
Meneja vipindi wa Redio Faraja na Mratibu wa Chemsha Bongo na Salome Makamba, Simeo Makoba.

“Maswali yanayoandaliwa katika Chemsha Bongo na Salome Makamba kwenye vipindi mbalimbali, hayaishi tu kuwawezesha kupata zawadi na badala yake yanaelimisha kuhusu masuala mbalimbali ambayo jamii yetu inakutana nayo katika Maisha ya kila siku”,ameongeza.

Amesema Chemsha Bongo na Salome Makamba imepokelewa kwa mwitikio mkubwa na wasikilizaji wa Redio Faraja waliopo ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga na inafuatiliwa kwa kina na watu kutoka maeneo mbalimbali kutokana na mbinu inayotumika kwani haina chembe chembe yoyote ya upendeleo wala udanganyifu katika kuwapata washindi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Redio Faraja Fm Stereo, Padre Anatoly Salawa ameshukuru na kupongeza ubunifu unaofanywa na Mbunge huyo na kwamba maswali yanayoulizwa kupitia Programu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba yanajenga jamii.

Kwa upande wao, baadhi ya washindi akiwemo Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu  Mkoa wa Shinyanga (SHIVYAWATA), Richard Mpongo amesema Mbunge Salome Makamba ni mbunge mwenye sifa za kipekee anayepaswa kuigwa kwani anagusa makundi mbalimbali katika jamii huku akiwataka wananchi kuchangamkia programu hiyo yenye manufaa kadha wa kadha.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Salome Makamba akizungumza leo Jumamosi Oktoba 21,2023 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa Washindi wa awamu ya tatu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba ambayo inaendeshwa na Redio Faraja kwa kushirikiana na Mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Salome Makamba. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Salome Makamba akizungumza leo Jumamosi Oktoba 21,2023 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa Washindi wa awamu ya tatu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Salome Makamba akizungumza leo Jumamosi Oktoba 21,2023 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa Washindi wa awamu ya tatu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba 

Mkurugenzi wa Redio Faraja Fm Stereo, Padre Anatoly Salawa akizungumza leo Jumamosi Oktoba 21,2023 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa Washindi wa awamu ya tatu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba

Meneja vipindi wa Redio Faraja na Mratibu wa Chemsha Bongo na Salome Makamba, Simeo Makoba  akizungumza leo Jumamosi Oktoba 21,2023 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa Washindi wa awamu ya tatu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu  Mkoa wa Shinyanga (SHIVYAWATA), Richard Mpongo  akizungumza leo Jumamosi Oktoba 21,2023 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa Washindi wa awamu ya tatu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba
Sehemu ya zawadi kwa Washindi wa awamu ya tatu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Salome Makamba akicheza muziki na akina mama
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Salome Makamba akikabidhi shilingi Milioni moja kwa Uongozi wa Stand United
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kushoto) akikabidhi jiko la Gesi kwa mmoja wa washindi wa awamu ya tatu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba

Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kushoto) akikabidhi jezi na mipira kwa Timu ya Mchicha FC kutoka Kolandoto washindi wa awamu ya tatu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba
Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba (kushoto) akikabidhi jezi na mipira kwa washindi wa awamu ya tatu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba

Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya madaftari na taulo laini kwa mwanafunzi mshindi wa awamu ya tatu ya Chemsha bongo na Salome Makamba

Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya madaftari kwa mwanafunzi mshindi wa awamu ya tatu ya Chemsha bongo na Salome Makamba

Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya tisheti kwa mmoja wa washindi wa awamu ya tatu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba

Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya shilingi 300,000/= kwa kikundi cha Wanawake cha wanawake wajasiriamali

Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Salome Makamba akikabidhi zawadi ya shilingi 300,000/= kwa kikundi cha Watu wenye ulemavu
Wadau wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Washindi wa awamu ya tatu ya Chemsha Bongo na Salome Makamba wakipiga picha ya kumbukumbu na viongozi mbalimbali

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com