Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Morogoro kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi.Neema Haule akizungumza wakati akifunga Mafunzo kwa waandishi wa habari waandamizi kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi
Na Kadama Malunde na Okuly Julius - Morogoro
Waandishi wa habari wameshauriwa kutumia vyema kalamu zao kutoa elimu kwa jamii kuhusu Sheria na Kanuni za ulinzi kwa watoa taarifa na mashahid ili wafahamu umuhimu wa kuwafichua wahalifu wa makosa mbalimbali yanayotendeka katika jamii kwa ajili ya kupunguza au kukomesha matukio ya kiuhalifu.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Morogoro Neema Haule Leo Oktoba 11,2023 Mkoani Morogoro wakati akifunga Mafunzo kwa waandishi wa habari waandamizi nchini kuhusu Sheria na Kanuni za ulinzi kwa watoa taarifa na mashahidi.
”Ni dhahiri kuwa, kwa muda huu mliopata mafunzo haya, mmeweza kufahamu vyema kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi. Rai yangu kwenu kama waandishi wa habari kupitia taaluma yenu ya habari muendelee kutoa elimu kwa umma wa watanzania kuhusiana na Sheria na Kanuni hizi kwa wananchi ili wafahamu umuhimu wa kuwafichua wahalifu wa makosa mbalimbali yanayotendeka katika jamii zetu ili mwisho wa siku matukio ya kiuhalifu yaweze kupungua na kuisha kabisa”, amesema Haule.
"Niwatakie kila la kheri katika majukumu yenu ya kuuhabarisha umma kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo Sheria na Kanuni za ulinzi kwa watoa taarifa na mashahidi na mkawe mabalozi kwa waandishi wa habari wengine katika vituo vyenu vya kazi, nao wajenge uelewa ili waweze kuifikisha elimu hii kwa jamii," ameongeza Haule.
Mafunzo hayo ya siku mbili (Oktoba 10 – 11,2023) Mkoani Morogoro yamekutanisha waandishi wa habari waandamizi kutoka mikoa mbalimbali nchini ambapo Wizara ya Katiba na Sheria imewapatia elimu kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi zenye lengo la kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya uhalifu kwa kuwatambua na kuwalinda watoa taarifa na mashahidi.
Kanuni hizo zitasaidia kuwapatia ulinzi wa kisheria wale wote wanaotoa taarifa za uhalifu wa makosa ya aina mbalimbali wanayoshuhudia yakitendeka katika jamii inayowazunguka.
Mafunzo hayo yametolewa kwa wanahabari waandamizi ili wawe mabalozi na kuihabarisha umma kuhusu taratibu za ulinzi kwa watoa taarifa na mashahidi ambapo wameelimishwa kuhusu Sheria ya Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi Sura ya 446 na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi, Kanuni zilizotolewa kupitia Tangazo la Serikali Namba 59 la tarehe 10, Februari 2023.
Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Morogoro kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi.Neema Haule akizungumza wakati akifunga Mafunzo kwa waandishi wa habari waandamizi kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi- Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Morogoro kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi.Neema Haule akifunga Mafunzo kwa waandishi wa habari waandamizi kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi
Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Morogoro kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi.Neema Haule akifunga Mafunzo kwa waandishi wa habari waandamizi kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi
Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Morogoro kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi. Neema Haule akifunga Mafunzo kwa waandishi wa habari waandamizi kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi
Mkurugenzi Msaidizi wa Katiba kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Burton Mwasomola akizungumza wakati wa Mafunzo kwa waandishi wa habari waandamizi kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi
Mkurugenzi Msaidizi wa Katiba kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Burton Mwasomola akizungumza wakati wa Mafunzo kwa waandishi wa habari waandamizi kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi
Wakili wa Serikali-Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Amani Manyaga akiwasilisha Mada kuhusu Sheria za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi katika Mafunzo kwa waandishi wa habari waandamizi kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog