Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC NAWANDA ATETA NA MAWAKALA WA USAFIRISHAJI ABIRIA STENDI KUU BARIADI



#AAGIZA UONGOZI HALMASHAURI YA MJI BARIADI KUIMARISHA USAFI,KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO YA VYOO KITUONI HAPO.

Bariadi,

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt Yahaya Ismail Nawanda amekutana na kuzungumza na Mawakala wa Usafirishaji katika eneo la Stendi kuu ya basi ya Mikoani Somanda Wilayani Bariadi.

Dkt.Nawanda anatembelea eneo hilo ikiwa ni utekelezaji wa ratiba yake ya kusikiliza na kutatua Kero mbalimbali za Wananchi 

Mawakala wa usafirishaji kituoni hapo wamemuambia Mkuu wa Mkoa Dkt.Nawanda  changamoto mbalimbali ikiwemo ubovu wa vyoo katika eneo hilo la Stendi.

Kutokana na changamoto hiyo Dkt.Nawanda ameuagiza Uongozi wa Halmashauri ya Mji Bariadi kishughulikia kwa haraka changamoto ya ubovu wa vyoo katika eneo hilo pamoja na kuimarisha Usafi wa Mazingira katika eneo hilo.

GCO,
Simiyu RS.
26 Oktoba 2023.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com