Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wa tatu kutoka kushoto Johari Samizi akiongozana na Mgeni Rasmi kuelekea Kanisani kwa ajili ya Shughuli ya harambee ya ujenzi wa Kibweta katika kanisa la Wasabato Lubaga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mh.Johari Samizi amewaomba viongozi wa dini Wilayani huko kuimairisha na kusimamia malezi kwa Watoto na jamii ili kuwa na taifa na waumini wenye hofu ya Mungu ambao watachangia kuendeleza taifa kwa kuwa lilipo fika ni uwepo wa kazi kubwa ya watumishi wa Mungu.
Samizi ameleeza hayo leo Jumamosi Oktoba 28,2023 wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Wadventista Wasabato Lubaga katika ibada maalumu ya harambee kwa ajili ya ujenzi wa kibweta cha Ghorofa tatu katika kanisa hilo kitakachokuwa na Shughuli mbalimbali.Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wa pili kutoka kulia Johari Samizi akiwa na Mgeni Rasmi wakati wakipokea salutiuelekea Kanisani kwa ajili ya Shughuli ya harambee ya ujenzi wa Kibweta katika kanisa la Wasabato Lubaga.Baadhi ya Vijana wa Kanisa hilo wakionyesha ishara ya ukakamavu mbele ya mgeni rasmi.Mgeni rasmi katika harambee ya ujenzi wa kibweta katika kanisa la waadvenstista wasabato Lubaga Nehemia Makindo akieleza nafasi na umuhimu wa kuchangia masuala ya kikanisa ambapo amechangia kiasi cha Shilingi Milioni 10 pamoja na mifuko ya saruji mia 500.
Samizi amesema Serikali inatambua na kuheshimu mchango mkubwa unaotolewa na viongozi wa dini katika kukuza na kutunza amani na mshikamano wa nchi,hali ambayo imechangia kuendelea kwa utulivu nchini ambapo amewataka kuendelea kuwakumbusha waumini wao wajibu wa kuwa na hofu ya Mungu.
Aidha Samizi amesema kumekuwapo na Mmomonyoko mkubwa wa
maadili kwa jamii ambao unachangiwa na wazazi kutokuwa na muda wa kutekeleza
majukumu yao iapsavyo ya malezi kwa kuwandaa Watoto kuwa wzazi bora wa kesho na kuwa bize shughuli za Maisha na kusaka
uchumi na kusahau malezi ya Watoto.
Samizi ameongeza kwa kusema kuwa wazazi na jamii
wanalojukumu kubwa la kuhakikisha wanalea Watoto katika msitari ulionyoka ili
kuwa na jamii, waumini na taifa lenye kumtukuza Mungu na kuwa na hofu pia.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amesema
halmashauri ya Manispa ya Shinyanga kazi yake kubwa ni kutoa huduma kwa jamii ambapo
amesema kanisa ni sehemu kubwa ya utekelezaji wa miradi ya kwa kuiasa jamii kuishi na kutenda katika
usawa.
Masumbuko amesema Viongozi wa Kiroho wana mchango kubwa katika maendeleo ya Manispaa
ya Shinyanga kwa kuelekeza, kufundisha na kuongoza waumini wao hali inayofanya
suala la utekelezaji wa miradi linakwensa pasipo kuwa na hofu.
Wakati huo Masumbuko amesema kila mmoja ana wajibu wa kutimiza
malengo yake ili kuhakikisha jamii inaishi vema.
Mgeni rasmi katika harambee hiyo ya ujenzi wa Kibweta
katika kanisa hilo Nehemia Makindo amesema kuwa jukumu la kujenga kanisa au
nyumba ya Mungu ni la kila muumini hivyo ni wajibu wao kulijenga kanisa.
Nehemia ameongeza kuwa pasipo kuijenga nyumba ya Mungu ni
kazi bure hivyo wao kama waumini wanapswa kusimama katika kujenga na
kuimairisha eneo la kuabudia ili waumini waweze kupata huduma za kiroho katika
eneo lenye amani.
Mchungaji aliyeongoza ibada ya harambee hiyo, Reward Mmbaga
amewataka watanzania na waumini kujenga utaratibu wa kutoa kwa kuwa kutoa kuna nguvu
kubwa ndani yake. (Luka 6:38).
Amesema kujenga utaratibu wa kutoa kuna nguvu kubwa na
kiwango kikibwa hivyo ni vema wauimini wakaujenga mfumo huo na kuwafundisha Watoto wangali wadogo
Ujenzi wa Kibweta hicho chenye Mimbari ya Kisasa,Kisima cha
ubatizo,Sehemu ya kubadili nguo kwa wabatizwa,Ofisi za Idara,Ofisi za Wazee wa Kanisa,Ofisi
ya Mchungaji,Ukumbi wa Mikutano,Studio ya Kisasa na Hosteli inataji kugharimu
shilingi Milioni mia sita hadi kukamilika kwake(600,000,000.) ambapo ujenzi huo
umegawanyika katika awamu tatu.
Aidha awamu ya kwanza ujenzi unataraji kugahrimu milioni
150 ikiwa ni ujenzi wa Msingi na Kunyanyua nguzo,awamu ya pili milioni 150
ikiwa ni ujenzi wa ghorofa ya kwanza nay a pili huku awamu ya tatu ikigharimu milioni 300 kwa ajili
ghorofa ya tatu,kuezeka,miundombinu na umaliziaji.
Katika harambee hiyo iliyofanyika leo October 28, 2023
katika kanisa la wadventista wasabato Lubaga jumla ya milioni 113,678,600
zimepatikana ikiwa keshi ni Milioni 56,446,100 huku ahadi ikiwa ni milioni 57,232,500.
Aidha jumla ya mifuko ya saruji 660 imepatikana katika
harambee hiyo, Mchanga tripu 34, Nondo 5 na Ng’ombe mmoja ikiwa ni sehemu ya
harambee hiyo ili kufikisha milioni 150 zinazohitajika katika ujenzi wa awali
wa Msingi na Nguzo za jengo hilo.
Baadhi ya Vijana wa Kanisa hilo wakionyesha ishara ya ukakamvu mbele ya mgeni rasmi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akitoa ahadi ya Milioni moja katika kuchangia ujenzi wa kibweta cha ghorofa tatu SDA Lubaga.