Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendesha Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Alhamisi Oktoba 5,2023 jijini Mwanza ambapo Wadau wa utangazaji (Redio na watoa huduma za utangazaji kwa njia ya waya).
Katika Programu hiyo ya utoaji elimu, wadau wa utangazaji wamepewa elimu kuhusu Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za kusimamia Huduma za Utangazaji za Kijamii, Mwongozo kwa watoa huduma za utangazaji kwa njia ya waya (Guideline for Cable Operators) na Mawasiliano na TCRA (Tanzanite Portal).
Akifungua mafunzo hayo, Meneja Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka amesema Watangazaji wana nafasi kubwa sana katika jamii hivyo ni vyema wakafanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii ili kuilinda jamii.
"Jinsi jamii tunavyoiona inatokana na mambo yanatotolewa kwenye vyombo vya habari, kama tunafanya vibaya basi pia tunaiharibu jamii, kama tunatengeneza vipindi vizuri basi tunajenga jamii bora. Mna nafasi kuwa sana ya kuitengeneza jamii hivyo ni lazima mtengeneze vipindi vya kujenga jamii ndiyo maana tunatengeneza kanuni za utangazaji ili jamii iendelee kuwa salama",amesema Mhandisi Kissaka.
"Teknolojia zinakuja lakini umuhimu wa Redio za kijamii unabaki pale pale hivyo ni muhimu mtambue kuwa nafasi yenu katika jamii ni kubwa sana",ameongeza Kissaka.
Kwa upande wake, Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amesema wametoa elimu kwa wadau wa utangazaji kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mhandisi Mihayo ametumia fursa hiyo kuwahamasisha watoa huduma za utangazaji kutumia zaidi mfumo wa kidigitali 'TCRA Tanzanite Portal' kuwa wasiliana kwa urahisi zaidi na mamlaka hiyo.
"Tunataka mtumie Digitali zaidi kuwasiliana na TCRA badala ya kutumia muda mwingi kuja TCRA. Tumieni mfumo wa Tanzanite Portal ili kuokoa gharama na muda wa kusafiri kufuata huduma, tunataka mtumie digitali kuwasiliana na TCRA. Ukitaka kuwasiliana na TCRA unaingia kwenye ukurasa wetu unaweka kile ambacho unataka sisi TCRA tukione",amesema Mhandisi Mihayo.
Katika hatua nyingine amewataka watangazaji kuzingatia maudhui wanayotoa kwenye vipindi kwa kuhakikisha wanatumia lugha nzuri ili kujenga jamii bora.
"Punguzeni sana kuchanganya lugha, mfano Kiingereza na Kiswahili lakini pia punguzeni kushabikia mambo ambayo hayako vizuri kwenye vipindi. Epukeni kushabikia masuala ya kisiasa. Usianze kutangaza kitu ambacho kina mkwamo kabla ya kuwasiliana na mamlaka husika mfano masuala ya matangazo ya Waganga wa kienyeji, tiba lishe, nguvu za kiume n.k", amesema Mhandisi Mihayo.
"Mwaka ujao ni mwaka wa uchaguzi, msishabikie masuala ya kisiasa, msinunulike, ukialika kiongozi wa chama cha siasa flani hakikisha unaalika na kutoka chama kingine, ukiona umealika mmoja mwingine hajaja acha hadi wawepo wote",ameongeza Mihayo.
Meneja Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka akizungumza wakati akifungua Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka akizungumza wakati akifungua Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii

Meneja Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka akitoa mada kuhusu Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za kusimamia Huduma za Utangazaji za Kijamii
Meneja Kitengo cha Huduma ya Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kissaka akitoa mada kuhusu Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za kusimamia Huduma za Utangazaji za Kijamii
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Programu ya utoaji elimu kwa wadau wa utangazaji Kanda ya Ziwa kuhusu Kanuni Mpya za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za Kusimamia Huduma za Utangazaji za Jamii

Mhandisi Mkuu kitengo cha Huduma za Utangazaji TCRA Mhandisi Jan Kaaya akiwasilisha Mada kuhusu Mwongozo kwa Watoa Huduma za Utangazaji kwa Njia ya Waya (Guideline For Cable Operators)
Mhandisi Mkuu kitengo cha Huduma za Utangazaji TCRA Mhandisi Jan Kaaya akiwasilisha Mada kuhusu Mwongozo kwa Watoa Huduma za Utangazaji kwa Njia ya Waya (Guideline For Cable Operators)
Afisa TEHAMA Mkuu TCRA, Irene Kahwili akiwasilisha mada kuhusu Mawasiliano na TCRA (Tanzanite Portal)

Mwenyekiti wa Umoja wa watoa huduma za utangazaji Tanzania (NIBA), Amos Ngosha akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Katibu wa Umoja wa watoa huduma za utangazaji Tanzania (NIBA), Heavenlight Kavishe akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Social Plugin