HABARI NJEMA KWA WAKAZI WA MANISPAA YA SHINYANGA NA WANANCHI
WOTE KWA UJUMLA.
Uongozi wa Hospitali ya LUCKMED iliyopo Kizumbi Bugayambele karibu na stendi ya mabasi ya mikoani Ibinzamata maarufu Manyoni na karibu na shule ya Little Treasures katika Manispaa ya Shinyanga, unayo furaha kubwa kuwatangazia wananchi wote kuwa kuanzia tarehe 27/10/2023 hadi 29/10/2023 kutakuwa na ujio wa madaktari bingwa kutoka hospitali ya Rufaa Bugando, hospitali ya rufaa ya Mkoa Shinyanga na hospitali ya Kolandoto watawaona, watawashauri na kuwatibu wagonjwa wa magonjwa mbalimbali ikiwemo na upasuaji
1. MADAKTARI BINGWA WA UPASUAJI watashughulika na uvimbe uliopo sehemu mbalimbali za mwili pamoja na:
I. Uvimbe sehemu yoyote kichwani
II. Uvimbe shingoni (maarufu kama Goita)
III. Uvimbe mdomoni na kwenye koo na Tonsesi
IV. Uvimbe tumboni na magonjwa ya kidole tumbo(appendix)
V. Uvimbe sehemu za siri na haja kubwa
VI. Ngiri za aina zote(Ngiri kavu(Henia) na Ngiri maji(Busha))
VII. Uvimbe mgongoni, mikononi na miguuni.
VIII. Uvimbe puani, nyama za puani na kushindwa kupumua
IX. Uvimbe kwenye mfuko wa kizazi
X. Uvimbe kwenye mfuko wa mayai ya uzazi
2. DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA AKINA MAMA NA UZAZI ATAKUWEPO.
3. DAKTARI BINGWA WA WATOTO ATAKUWEPO
4. DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA NDANI ATAKUWEPO
Wagonjwa wenye matatizo ya moyo, sukari, figo, vidonda vya tumbo wataonwa.
5. DAKTARI WA MAZOEZI YA VIUNGO atakuwepo.
6. PIA MADAKTARI BINGWA WENGINE WATAKUWA WANATIBU WAGONJWA
WAFUATAO;
I. Wagonjwa walioshindwa kukojoa
II. Wagonjwa wenye maumivu ya tumbo ya aina yoyote
III. Wagonjwa walio jisokota utumbo na kushindwa kupata haja kubwa
IV. Wagonjwa waliovunjika mikono na miguu
V. Wagonjwa wenye matatizo ya uzazi, macho na miguu.
VI. Wenye uhitaji wa miwani itakuwepo
VII .Huduma ya kupima presha na saratani ya matiti zitatolewa bure.
Namna ya kujiandikisha fika Hospitali ya Luckmed iliyopo Kizumbi Bugayambelele
karibu na shule ya Little Treasures.
Utaandikisha jina lako na tatizo
linalokusumbua. Kwa wale ambao mko mbali au ambao hamtaweza kufika tuma
ujumbe wasms au piga no 0763-979758/0682-407676/0767-211531/0753-
829014/0762-311531 mwambie ushiriki wako, jina na tatzo linalokusumbua kwa
ajili ya kuhudumiwa.
Na kwa wale watakaokuja siku hiyo ya tukio watapokelewa.
AFYA YAKO NDIO KIPAUMBELE CHETU;
WOTE MNAKARIBISHWA KWA HUDUMA BORA ZA MATIBABU
.
……………………..AHSANTENI…………………….
Social Plugin