Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu ajira, kazi vijana na watu wenye ulemavu Prof.Joyce Ndalichako akiwavisha nishani vijana 23 waliopanda mlima Kilimanjaro leo Mjini Babati na amewavisha nishani baadhi ya viongozi wa wizara. Picha: JALIWASON JASSON
****
Na Jaliwason Jasson, BABATI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira, Kazi, Vijana na Watu wenye ulemavu Prof. Joyce Ndalichako amewakabidhi nishani na zawadi ya fedha sh. 300,000 kila kijana vijana 23 wazalendo waliopanda mlima Kilimanjaro na kutembea kutoka Arusha mpaka Babati.
Prof. Ndalichako ametoa nishani hizo na zawadi leo baada ya kukimbia kilometa 3.5 na vijana hao.
Amewataka vijana kuwa waadilifu kwa kuwa uadilufu ni silaha kubwa na wakikopeshwa na Benki wanatakiwa kurejesha ili kutoa fursa kwa vijana wengine.
Amewaomba vijana kuendelea kuiunga mkono serikali ili iendelee kuwainua kiuchumi kupitia fursa zilizopo.
Naye Omari Kusaka ameishukru serikali kwa kutambua mchango wa vijana na kuendelea kuwaunganisha na fursa za kiuchumi.