Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TCRA YABAINI MADUDU KWENYE KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI, YATAKA WAANDISHI WAPEWE SANA MAFUNZO

Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis akizungumza wakati wa Usiku wa Wadau wa Habari na Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imebaini kuwa Waandishi wa Habari wengi katika Klabu za Waandishi wa Habari (Press Clubs) hawajui sheria za sekta wanayoifanyika kazi hivyo kuomba Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini (UTPC) na wadau wengine waendelee na juhudi za kuzijengea uwezo wa kimafunzo klabu hizo za waandishi wa habari.

Hayo yamesemwa Ijumaa Oktoba 20,2023 na Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo wakati wa Hafla ya Usiku wa marafiki na wadau wa vyombo vya habari Kanda ya Ziwa (Lake Zone Media Stakeholders Night Gala 2023) ikiongozwa na kauli mbiu ya ‘vyombo vya habari imara ni chachu ya maendeleo ya nchi’ iliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.

Mhandisi Mihayo amesema baada ya TCRA kuendesha mafunzo kuhusu ya sheria za habari kupitia Klabu za Waandishi wa Habari mikoa yote ya Kanda ya Ziwa imebaini mambo kadha wa kadha ikiwemo Wanachama wengi wa klabu hizo kutojua sheria za sekta wanayoifanyika kazi.

Amesema pia TCRA imebaini kuwa baadhi ya waandishi wa habari kuwa wavivu wa kutafuta habari na hivyo kuwa na makosa yanayofanana kwenye vyombo vya habari lakini pia baadhi ya vituo vya redio kuwa na watangazaji wanaotumia lugha mchanganyiko (Kiswahili na Kiingereza).
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo. 

“Jambo jingine tulilolibaini ni baadhi ya wanachama wa Klabu za waandishi wa habari kuwa chanzo cha kuvunja sheria kwa kuendesha vituo vya habari mtandaoni bila kuwa na leseni kutoka TCRA pamoja na umuhimu mdogo wa kujiendeleza kielimu kwa waandishi wa habari”,amesema Mhandisi Mihayo.

Amezitaja changamoto zingine zilizojitokeza ni mpasuko miongoni wa wanachama wa klabu hizo, ukosefu wa ubunifu kwenye baadhi ya Klabu za waandishi wa habari na idadi ndogo ya wanachama.

"Mambo mazuri yaliyojitokeza ni pamoja na uhitaji wa waandishi kuwa wanachama wa press clubs ni mkubwa lakini pia Viongozi wa serikali na wadau mbalimbali wana utayari mkubwa wa kuzisaidia klabu , baadhi ya klabu kuwa tayari kubadilika ili ziwe imara",ameeleza.

“Mambo mengine tuliyobaini ni Wanachama wengi wa klabu za waandishi wa habari kuwa na shauku ya kuanzisha blogs zao wenyewe na Waandishi wengi wapo kuwa tayari kujifunza sheria za sekta za habari ili waweze kufanya kazi kwa weledi na usalama”,ameongeza.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko (kushoto) akimkabidhi Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo cheti cha shukrani ya kuwa mdau mkubwa wa Klabu hiyo

Amesema TCRA inapendekeza UTPC na wadau wengine waendelee na juhudi za kuzijengea uwezo wa kimafunzo Klabu za Waandishi wa habari na Klabu hizo zijenge utaratibu wa kuandika maandiko ya miradi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, zijenge tabia ya kutembeleana kwa nia ya kubadilishana uzoefu na kujifunza na zile zenye tofauti UTPC itafute njia sahihi ya kupunguza au kumaliza kabisa tofauti za klabu hizo.

“TCRA itaendelea kufuatilia uendeshaji wa vipindi ili kuhakikisha kuwa masharti ya leseni yanatekelezwa. TCRA inatoa wito kwa wale wote wanaomiliki, kuendesha na kutoa huduma mtandaoni kama blogs, Youtube channel na Radio mtandao zisizosajiliwa wafuate taratibu ili waweze kuzisajili”,ameongeza.

Kwa upande wake, Mgeni rasmi wakati wa Hafla hiyo, Katibu Tawala Wilaya ya Ilemela, Mariam Msengi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilemela kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makala amevipongeza vyombo vya habari kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuihabarisha jamii pamoja na kutangaza kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko ameishukuru na kuipongeza TCRA kwa kutoa mafunzo ya sheria za habari kwa waandishi wa habari katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwani ili waandishi wa habari wafanye kazi zao vizuri wanapaswa kuzijua sheria zinazoongoza tasnia ya habari.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Usiku wa Wadau wa Habari na Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa katika ukumbi wa Mwanza Hotel Jijini Mwanza Oktoba 20,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis akizungumza wakati wa Usiku wa Wadau wa Habari na Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa katika ukumbi wa Mwanza Hotel Jijini Mwanza Oktoba 20,2023.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Usiku wa Wadau wa Habari na Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa 

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Katibu Tawala Wilaya ya Ilemela, Mariam Msengi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makala wakati wa Usiku wa Wadau wa Habari na Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko akizungumza wakati wa Usiku wa Wadau wa Habari na Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa 
Wafanyakazi wa TCRA wakitambulishwa wakati wa Usiku wa Wadau wa Habari na Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa
Wafanyakazi wa TCRA wakitambulishwa wakati wa Usiku wa Wadau wa Habari na Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa
Wafanyakazi wa TCRA  na wadau wakiwa kwenye Usiku wa Wadau wa Habari na Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa
Wafanyakazi wa TCRA  na wadau wakiwa kwenye Usiku wa Wadau wa Habari na Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa
Wafanyakazi wa TCRA  na wadau wakiwa kwenye Usiku wa Wadau wa Habari na Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko (kushoto) akimkabidhi Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo cheti cha shukrani ya kuwa mdau mkubwa wa Klabu hiyo
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo (kulia) na viongozi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea ukumbini
Wadau wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea ukumbini
Wadau wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea ukumbini
Wadau wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea ukumbini
Burudani kutoka kwa Mwanamuziki Mwinjuma Muumini ikiendelea wakati wa Usiku wa Wadau wa Habari na Vyombo vya Habari Kanda ya Ziwa.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com